• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

'Nala Lorry Park' suluhisho la maegesho Jijini Dodoma

Imewekwa tarehe: February 20th, 2021

KITUO kikuu cha kuengesha malori kilichopo eneo la Nala (Nala lorry park) kimeanza kazi na kuwavutia wadau wa sekta ya usafirishaji ndani na nje ya Jiji la Dodoma.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru mapema leo tarehe 20 Januari, 2021 majira ya saa 11 alfajiri alifanya ziara ya kikazi kujionea hali halisi ya kituo kikuu cha kuegesha malori- Nala. Katika ziara hiyo, Mkurugenzi huyo aliridhishwa na utendaji kazi wa kituo hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alisema kuwa kituo hicho cha kuegesha malori ni mkakati wa serikali katika kutoa huduma bora kwa wadau wa sekta ya usafirishaji na wananchi kwa ujumla. Alisema kuwa baada ya kukamilika kwa kituo hicho, malori yote hayaruhusiwi kuegeshwa na kuzagaa katika jiji la Dodoma.

“Kituo cha kuegesha malori Nala kimekamilika, ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya tano, hivyo, malori yote yanatakiwa kupati katika kituo kile. Madereva watakao kaidi utekelezaji huo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu zilizopo” alisema Fungo.

Akiongelea huduma za kijamii, mkuu huyo wa kitengo cha TEHAMA alisema kuwa tayari huduma mbalimbali zinapatikana katika eneo la kuzunguka kituo hicho. Miongoni mwa huduma zilizopo ni pamoja na usafiri wa aina mbalimbali, huduma za kijamii na chakula, aliongeza.

Kwa upande wake, mdau wa sekta ya usafirishaji ambaye ni dereva wa lori, Erenest Sangu alisema kuwa kutuo cha kuegesha malori- Nala ni kituo bora nchini. Kituo hicho kinawapa uhakika na usalama wa malori na mizigo yao kwa sababu eneo hilo limeimarishwa kiusalama, iliongeza.

Kituo kikuu cha kuegesha malori kimejengwa katika Kata ya Nala, jijini hapa kikiwa barabarani katika barabara kuu iendayo Singida umbali wa takribani kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma.

Mwonekano kutoka angani wa Kituo cha kuegeshea malori Nala.






Huduma ya usafiri wa chap chap 'bodaboda' inapatikana Nala Lorry Park.

Matangazo

  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 - Awamu ya Pili February 19, 2021
  • Tangazo la Mnada wa Hadhara February 15, 2021
  • Matokeo ya Kidato cha Nne, cha Pili na Darasa la Nne 2020 haya hapa January 15, 2021
  • Zoezi la upandaji miti watumishi wote January 15, 2021
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Dodoma Jiji FC yaipiga Kipigwe FC 7 - 0

    February 28, 2021
  • Wizara ya Afya kutumia panyabuku kubaini Kifua Kikuu

    February 26, 2021
  • Mshambuliaji Anwary Jabir aweka rekodi ligi kuu, 'apewa' uchezaji bora

    February 25, 2021
  • Jiji katika opesheni ya kujiimarisha kimapato

    February 25, 2021
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata kusimamia usafi wa mazingira katika kata zao
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    3 CDA Street

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.