Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, anawatangazia wananchi wote kuwa zoezi la Anuani za Makazi na Postikodi bado linaendelea katika Mitaa yote ya Jiji la Dodoma.
Mwananchi ambaye hajapitiwa na zoezi la Postikodi na Anuani za Makazi na ambaye hatakuwepo katika kaya wakati zoezi hilo linapoendelea, anapaswa kuacha nyumbani nakala ya Kitambulisho cha Taifa au Namba ya NIDA pamoja na namba ya Simu ili kurahisisha kufanikisha zoezo hilo.
Aidha, anaweza kwenda Ofisi ya Mtendaji wa Kata yake kujaza fomu maalum ili taarifa zake ziweze kuingizwa kwenye Mfumo wa Anuani za Makazi.
Mwananchi unaombwa kutoa ushirikiano kwa Maafisa waandikishaji wanapofika katika kaya yako kabla ya tarehe 05/05/2022.
Tangazo hili limetolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.