Sunday 22nd, December 2024
@Nyerere Square
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, anawatangazia wananchi wote kuwa kesho tarehe 27/08/2019 litafanyika zoezi la utiaji saini mikataba ya ujenzi wa majengo mawili ya vitegauchumi vya Jiji.
Mkataba wa kwanza ni ujenzi wa Hoteli ya Jiji la Dodoma (Dodoma City Hotel) katika Mtaa wa Nyerere. Mkandarasi ni Stecol Coorporation (China) kwa gharama ya mradi Sh. Bilioni 9.995.
Mkataba wa pili ni ujenzi wa Jengo la Kitegauchumi cha Jiji (Government City Complex) katika mji wa Serikali Mtumba. Mkandarasi ni Mohamed Builders Ltd (Tanzania) kwa gharama ya mradi Sh. Bilioni 59.3.
Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Seleman Said Jafo (Mb).
Zoezi hilo la wazi la utiaji saini Mikataba ya ujenzi wa vitegauchimi litafanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma, kuanzia Saa 4:00 asubuhi.
Ujenzi wa vitegauchumi hivyo utatumia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji.
Wananchi wote mnaalikwa kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Limetolewa na:
Joseph E. Fungo
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na UHUSIANO
Halmashauri ya Jiji
DODOMA
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.