Na. Sofia Remmi, DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amepokea na kukabidhi vifaa vya michezo, vya kujifunzia pamoja na vitendea kazi vya watoa huduma za afya ngazi ya Jamii ili viweze kuwafikia walengwa waliopo katika baadhi ya halmashauri za mkoa huu.
Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jengo la Mkapa.
Akizungumza na baadhi ya wadau na watoa huduma ngazi ya jamii amesema Mkoa unashirikiana na Shirika la Action for Community Care (ACC) katika kutekeleza miradi ya Imarisha Afya na ViiV Pediatric Breakthrough Partnership ambayo inalenga kusaidia watoto na vijana wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wenye umri wa miaka 0-19. Miradi inawezesha kuwaibua na kuwaunganisha watoto na vijana kwenye matibabu, kuwasaidia kubaki katika huduma na matibabu na kuishi maisha yenye afya.
“Vifaa vya michezo na vya kujifunzia vinavyopokelewa leo vina umuhimu wa kipekee kwa kuwa vitawezesha uchangamshi na ukuaji wa ubongo wa watoto na kuwamotisha watoto na vijana kuhudhuria kliniki kwa ajili ya huduma za VVU na kupunguza utoro na kuamasisha watoto dhidi ya kujifunza zitaongeza hamasa kwa wazazi na walezi kuwaleta watoto kwenye vituo vya tiba na matunzo hivyo, wakati wakisubiri huduma watoto na vijana watajifunza baadhi ya mambo badala ya kukaa bila kufanya kitu” alisema Senyamule.
Miradi hii ililenga pia kuwatambua na kutoa mafunzo kwa Wakunga wa Jadi kwa lengo la kuwaelekeza kuhusu umuhimu wa kuwaelimisha wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa usalama wao na watoto watakaozaliwa.
Kwa upande wake Meneja wa Miradi, Merina Mgongo alisema ACC ni shirika lisilo la Kiserikali na linatekeleza shughuli zake katika Halmashauri nne za Mkoa wa Dodoma ikiwemo Kongwa, Chamwino, Mpwapwa na Dodoma Mjini.
“ACC inateleza miradi ya Afya, Elimu, Kuboresha vifaa vya michezo Kama Bembea za watoto, mipira ya miguu na mkono, kikapu, kamba za kuruka, midoli, vinanda, runinga na vinginevyokuimarisha katika ngazi ya jamii na mazingira” alisema Mgongo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.