SHIRIKA la Agakhan @agakhanhospitaldsm limetoa bidhaa za Afya na vifaa vya kujikinga na maambukizi (Personal Protectove Equipment) dhidi ya ugonjwa wa homa ya Nyani (M - POX) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 200.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa kwenye kituo cha Afya Ikwiriri Kilichopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Afisa Uhusiano wa Agakhan Bw. Juma Dosa amesema wameamua kuunga mkoni jitihada za Waziri Mchengerwa za kuboresha Afya za Wanarufiji na kwa kufanya hivyo wamekuja na bidhaa za Afya na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ta shilingi Mil. 200 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya M-Pox.
Bw. Dosa aliongeza kuwa misaada hiyo ileenda sambamba na huduma za uchunguzi wa magonjwa ya Kansa ya ziwa, mlango wa kizazi pamoja na Tezi Dume hapa Ikwiriri na huduma hizo zitatolewa bura kwa muda wa siku 2.
Akizungumza baada ya kupokea bidhaa za Afya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewashukuru Aghakan kwa mchango wao katika huduma za Afya Rufiji na ametaka wananchi wa Rufiji kutumia fursa hiyo kufika kwenye Kliniki kwa ajili ya uchunguzi wa Afya zao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.