• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Alhaj Shekimweri ahamasisha umuhimu wa mazoezi kwa wachezaji Dodoma Jiji FC

Imewekwa tarehe: January 29th, 2025

Na. Coletha Charles, DODOMA

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, ameitembelea Timu ya Dodoma Jiji FC, inayondelea na mazoezi ya maandalizi ya msimu wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa lengo la kuwahamasisha wachezaji na viongozi wa timu kwa ajili ya kujiandaa vema.

Akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu kwenye uwanja John Merlin, Mkuu wa Wilaya alisisitiza umuhimu wa maandalizi mazuri kwa ajili ya msimu wa pili wa ligi kuu na kuwataka wachezaji kufanya mazoezi ili kuhakikisha wanapata mafanikio.

Alisema kuwa, wanatakiwa kuweka mikakati yenye uhalisia kwa sababu wanaenda kwenye kipindi kibaya ambapo kusipokuwa na utulivu na maelewano wataishia kulaumiana na kushutumiana. “Tunaenda ‘second round’ ya ligi yetu hatuko sehemu nzuri sana, hatuko sehemu mbaya sana katika mechi 16 nafikiri tuna ‘point’ 19 wastani wa ‘point’ moja kwa kila mechi. Kwahiyo, kuna haja ya kuwa familia moja kama alivyoongea mwalimu kwa kuelewa nini kipo mbele yetu. Tuna mechi 14 tu za kujua hatima yetu na ‘kuadjust’ malengo yetu” alisema Alhaj Shekimweri.

Kwa upande wake, Kocha wa Dodoma Jiji FC, Mecky Maxime, alithibitisha kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wanajipanga kufanya vema katika mechi. Lakini pia aliomba ushirikiano katika kipindi cha msimu wa pili wa ligi kuu. “Tuna maingizo mawili ya wachezaji wapya ambayo tumeingiza, lakini sasa hivi tunaenda kipindi kibaya sana na kina athari kwetu sisi, ukiangalia kwenye maandalizi tuko wengi, lakini hapa yakianza kutokea matokeo kunakikundi kingine kinajitenga, kikundi kingine kinabeba mzigo. Hivyo, siyo kipindi rahisi, nimechi ngumu, tunakwenda tutacheza na Pamba hapa (nyumbani) halafu tunamechi mbili nje” alisema Maxime.

Nae, Nahodha wa Dodoma Jiji FC, Augustino Nsata, alieleza kuwa maandalizi ya msimu huu yanaenda vizuri na wanajiandaa kuonesha kiwango cha juu kwenye mechi zijazo. “Maandalizi yetu yanaendelea vizuri na tunatarajia kufanya vizuri katika mechi. Sisi kama wachezaji tumejiandaa na tunajua tunamichezo migumu mbele yetu tunachoshukuru Mungu hatuna majeraha kila mtu yupo tayari kupambania nembo ya timu yetu ili kuhakikisha tunafanya vizuri” alisema Nsata.

Ikumbukwe kuwa, Dodoma Jiji FC imesajili wachezaji wawili Abdi Banda kutoka FC Baroka ya Afrika Kusini na Mukrim Issa ambaye amejiunga kwa mkopo kutoka klabu ya Singida BS. Pia timu hii ina malengo ya kufanya vizuri zaidi kwenye msimu huu wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na inaendelea na maandalizi yake kwa umakini ili kufikia malengo hayo.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.