Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amewahimiza wanachama wa Ardhi SACCO Ltd. kuongeza ubunifu zaidi ili kuleta hamasa ya maendeleo na kuwavutia wanachama wengi zaidi kujiunga na Chama hivyo.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Mhandisi Sanga Desemba 14, 2023 jijini Dodoma wakati wa kufungua Mkutano wa Mwaka wa Ardhi SACCOS, Mkurugenzi wa Idara ya Milki Wizara hiyo Dkt. Upendo Matotola amewataka wanachama hao kufanyakazi kwa bidii ili kufikia malengo ya SACCOS hiyo.
"Mkiweza kujiunga wote na Chama hiki, niwahakikishie mtapiga hatua kubwa sana katika kukabiliana na makali ya maisha pamoja na kujikwamua kiuchumi kama watumishi" amesema Dkt. Matotola.
Kwa sasa Chama hicho kina wanachama 354 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo kulikuwa na wanachama 295 tangu SACCOS hiyo ianzishwe mwaka 2021 huku Wizara hiyo ikikadiriwa kuwa na watumishi takriban 2,300.
Aidha, Dkt. Matotola ameongeza kuwa, kila mwanachama anawajibu wa kuwa balozi na kuhamasisha watumishi wengine wa Wizara hiyo kujiunga na Chama hicho.
Akitoa taarifa ya Chama hicho Bw. Godfrey Machabe,amesema kuwa malengo ya Ardhi SACCOS Ltd ni kuwawezesha watumishi wa Wizara hiyo kujikwamua kiuchumi katika maisha yao ya kila siku.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.