KAZI ya upimaji wa eneo lote la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka miwili ijayo hali itakayoufanya mji wa Dodoma kuwa katika mandhari bora na ya kuvutia.
Mpango huo umewekwa wazi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alipozungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Manispaa juzi.
Alisema miradi ya upimaji wa ardhi katika utekelezwaji wa lengo hilo haitafanywa na Manispaa pekee bali itashirikisha taasisi mbalimbali zenye uzoefu wa miradi ya aina hiyo.
Alifafanua kuwa, mbali na kushirikisha taasisi za Umma na binafsi, Manispaa ya Dodoma ina mkakati wake wa upimaji na tayari baadhi ya Kata zimeshaanza kupimwa ambapo pia, upo mkakati wa kuongeza nguvu kazi kwa upande wa watumishi kwa kuajiri wataalamu wa ardhi kwa mikataba ya muda ili kufikia lengo lililowekwa kwa wakati.
Manispaa ya Dodoma inaundwa na Kata 41, ambapo ina jumla ya eneo la mraba 2,769, ambapo zaidi ya nusu ya eneo hilo bado halijapimwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.