• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma launga mkono maono ya Rais Dkt. Samia Nishati safi

Imewekwa tarehe: February 1st, 2025

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inaunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha nishati safi kwa wote inapatikana kwa lengo la kuboresha maisha ya watanzania.

Kauli hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitia mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/ 2026 mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Prof. Mwamfupe alisema “sisi Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma tunatoa pongezi kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa nishati safi. Mwanzo mwa wiki hii dunia yote macho yalikuwa Tanzania kwa ajili ya mkutano wa nishati kwa ajili ya afya kwa manufaa ya wananchi wetu na mazingira bora. Dodoma ni wanufaika wakubwa wa dhana hiyo kwasababu miti yetu itabaki salama. Sisi ni waungaji mkono namba moja wa dhana hii”.

Aliipongeza Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kusema kuwa mchakato ulikuwa shirikishi na umechukua nafasi yake. Nafahamu mchakato ulipita katika vikao vyote vya kisheria kama Baraza la Wafanyakazi la Jiji la Dodoma na Kamati ya Ushauri ya Wilaya. “Niwakumbushe tu kuwa bajeti siyo mpango wa matumizi pekee, inahusu mpango wa mapato. Hivyo, tupo hapa kujadili na kupitia mapendekezo ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2025/2026” alisema Prof. Mwamfupe.

Awali akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Francis Kaunda alisema kuwa bajeti hiyo imeongezeka kwa asilimia saba. “Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji naomba kuwasilisha rasimu ya makisio ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kuwa ni jumla ya shilingi 147,910,202,949. Kati ya fedha hizo shilingi 67,385,000,000ni mapato ya ndani, shilingi 65,739,308,000 ruzuku ya mishahara, shilingi 3,071,349,000 ni ruzuku ya matumizi mengineyo na shilingi 11,714,545,949 ruzuku ya miradi ya maendeleo. Hivyo, bajeti imeongezeka kwa asilimia 7.04 ukilinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025” alisema Kaunda.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipitisha kwa kauli moja mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 jumla ya shilingi 147,910,202,949.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.