Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli leo Jumamosi Disemba 5, 2020 amefanya uteuzi wa Mawaziri 21 na Naibu Mawaziri 23 huku akiwateua waliokuwa makatibu wakuu wa wizara kuwa wabunge na kisha kuwateua kuwa mawaziri.
Aidha, Rais Dkt. Magufuli ameanzisha Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kumteua Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile kuwa Waziri wa wizara hiyo na Kundo Mathew kuwa naibu waziri wake.
Akitangaza uteuzi huo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema uteuzi wa mawaziri wawili, Profesa Palamagamba Kabudi (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki) na Dkt. Philip Mpango (Fedha na Mipago) unaendelea na hivyo kufanya idadi ya mawaziri kuwa 23 na naibu mawaziri 23.
Walioteuliwa kuwa Wabunge na kisha uwaziri ni Dkt. Dorothy Gwajima aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Tamisemi akishughulikia sekta ya Afya pamoja na Dkt. Leonard Chamuriho ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi.
Walioteuliwa kuwa Mawaziri:
Naibu Mawaziri:
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.