• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Bashe akemea vikali Wakulima wanaouza namba za siri

Imewekwa tarehe: November 24th, 2022

WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amewakemea vikali wakulima wanaowauzia wafanyabiashara namba zao za siri kwa ajili ya kupata mbolea za ruzuku kwa njia za udanganyifu.

Bashe alizungumza hayo wilayani Kondoa alipopewa nafasi na Mh Rais Samia Hassan Suluhu akiwa ziarani kuelekea Mkoani Manyara.

Waziri Bashe amesema wakati serikali ya Awamu ya Sita inafanya kila jitihada kuwapunguzia wakulima gharama ya mbolea, baadhi yao wanahujumu jitihada hizo.

Akitoa mfano Waziri huyo wa kilimo amesema wakulima wapatao 20 mkoani Kigoma wamekamatwa kwa tuhuma za kuwauzia wafanyabiashara wa mbolea namba zao za siri kwa ajili kupata mbolea za ruzuku.

"Napenda kuwafahanisha wakulima wote nchini kuwa mfumo tunaotumia kutoa mbolea za ruzuku ni wa kidigitali, hivyo chochote kinachofanyika katika mfumo huo tunakifahamu", alisema Bashe.

Amewaonya wote watakaojihusisha na vitendo vya udanganyifu ili kuhujumu mpango wa serikali wa utoaji mbolea za ruzuku kuwa watachukuliwa hatua kali.

Waziri Bashe amewataka wakulima kununua mbolea kwa bei za ruzuku zilizowekwa na serikali ili kuwapunguzia makali ya pembejeo hiyo muhimu.

Akizungumzia kuhusu uuzaji wa mazao, Bashe amesema serikali imetoa ruhusa kwa wakulima kuuza mazao yao mahali popote na kuacha ziada itakayotumika kama chakula. 

Amesema kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, mwaka huu kuna mvua kidogo hivyo amewataka wakulima kutumia mvua za kwanza kupandia na kulima mazao yanayostahimili ukame kama vile mihogo na mtama.

Aidha amempongeza Rais Samia kwa utashi wake wa kisiasa wa kuwekeza zaidi kwenye sekta ya Kilimo, ambapo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, wizara yake imepatiwa kiasi cha takribani Tsh. billioni 900

 Amesema uwekezaji mkubwa uko katika kujenga miundombinu ya umwagiliaji ambayo pia itatumika kwa ajili ya kuandaa mbegu za alizeti zitakazotolewa kwa bei ya ruzuku.

Waziri Bashe amewahakikishia Watanzania kuwa hakuna mtu atakayekufa kwa njaa kwani serikali ina chakula cha kutosha.

" Tayari tumepeleka chakula katika halmashauri 41 ili wananchi wauziwe kwa bei nafuu", Alisema Bashe.





Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.