• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Bashungwa aagiza mikoa, halmashauri kutangaza miradi ya maendeleo

Imewekwa tarehe: July 2nd, 2022

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza viongozi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanawatumia Maafisa Habari katika kuhabarisha umma kuhusu kazi zinazofanywa na Serikali.

Ametoa Kauli hiyo leo tarehe 2 Julai, 2021 wakati akifungua kikaoa kazi cha Maafisa Uhusiano wa Taasisi, Maafisa Habari wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, Jijini Dodoma.

Bashugwa amesema kuwa ni wajibu wa Viongozi hao kuhakikisha wanaitumia Timu ya Maafisa Habari nchini kutangaza miradi ya Maendeleo inayotekelezwa nchi nzima ili kuwapasha habari wananchi na kuwawezesha kuelewa kazi kubwa inayofanywa na Serikali yao.

“Suala la Kuhabarisha Umma ni la kufa na kupona kuhusu utendaji kazi wa Serikali kwa watanzania ni muhimu, si jambo la hiari bali ni lazima kuhabarisha umma juhudi za Serikali katika kuwatumikia wananchi," amesitiza Waziri Bashungwa.

Amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya, wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika mwaka wa fedha 2022/2023 kuhakikisha wanatoa habari kuanzia ngazi ya Kijiji , Mtaa, Wilaya, Mikoa na Taifa kwa ujumla ili kila mtanzania aweze kujua kazi zilizofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Pia, Bashungwa amewataka viongozi hao kuhakikisha wanawasimamia Maafisa Habari wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuhabarisha umma kwa wakati kwa kuzingatia sheria, taratibu na Miongozo ya Utumishi wa umma.

Amesema kuwa Maafisa Habari wote nchini wakitimiza majukumu yao kwa weledi kutasaidia kuuhabarisha umma kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao na kujua kazi iliyofanywa na Serikali katika Kuleta maendeleo.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde amewataka Maafisa Habari wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi na muhimu ambazo serikali inawafanyia.

Aidha, Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Gerson Msigwa amewataka Maafisa habari wote nchini kutumia radio na television za kijamiii katika maeneo yao kutangaza mafanikio na agenda ya kitaifa ili kuweza kuisaidia Serikali.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.