WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa asilimia 23.3.
Akitoa salamu za Ofisi ya Rais - TAMISEMI leo tarehe 18 Mei, 2022 kwenye uzinduzi wa barabara ya Tabora - Koga - Mpanda yenye urefu wa kilometa 342.9, uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Mkoani Tabora. Waziri Bashungwa amesema asilimia 75 ya watumishi wanaotoka kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa watafaidika na amemuahidi Rais kufanyakazi kwa weledi katika kuwatumikia wananchi.
Waziri Bashungwa pia amemshukuru Rais Samia Suhulu Hassan kwa kuongeza bajeti ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge hadi kufikia asilimia 193 na kubadilisha mandhari ya eneo hilo.
Bashungwa anaendelea kufafanua kuwa kwa upande wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Sikonge, Serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya.
Amesema kwa upande wa ujenzi wa kituo cha afya, Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Tuturo na kwa upande wa utatuzi wa changamoto ya ujenzi wa nyumba za walimu nchini katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 55.57 kwa ajili ya ujenzi huo.
Akifafanua zaidi Bashungwa amesema kwa upande wa ujenzi wa jengo la utawala, Serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 700 na katika bajeti yam waka 2022/23 zimetengwa shilingi milioni 600 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la utawala ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la anwani za makazi na kujitokeza kuhesabiwa ili Serikali iweze kuwatambua na kuweza kutoa huduma bora kulingan na takwimu zilizopo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.