• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Bashungwa awataka ma-RC kujifunza Dodoma Jiji

Imewekwa tarehe: March 12th, 2022

WAKUU wa Mikoa yenye Halmashauri zenye hadhi ya Majiji wametakiwa kutumia mbinu inayotumika katika ujenzi wa Soko la Wafanyabiashara wadogo (Machinga Open Market) katika eneo la Bahi Road jijini Dodoma ili kuboresha zoezi la upangaji wa machinga kulingana na mazingira ya maeneo yao.

Wito huo umetolewa leo tarehe 12 Machi, 2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa wakati wa ziara yake na wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala, na Wakurugenzi wa mikoa yenye hadhi ya majiji kutembelea ujenzi wa eneo hilo.

Akizungumza na viongozi hao, Bashungwa alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametambua sekta ya machinga kuwa rasmi hivyo kwa sasa wanaenda na maono yake ya kuhakikisha wanajengewa mazingira rafiki kwa kazi zao.

“Hapo awali changamoto ya machinga haikuwa na suluhu kwa sababu tuliyokuwa tunatafanya kuzitatua hayakuwa na uhalisia, hivyo kwa soko letu hapa baada ya maelekezo ya Rais kuwajengea mazingira rafiki tukaamua kutokwenda nje ya nchi kuiga wenzetu wanavyofanya tukathamini vya ndani kwa kwenda eneo la Mnadani Msalato jijini hapa ili kuona ni namna gani watafanya biashara zao".

Napongeza ubunifu uliofanyika kwenye soko hili la machinga na namna jiji lilivyotafsiri maono ya Rais kwa kubuni masuala haya hii ni fursa kwa viongozi wengine wa mikoa yenye hadhi ya majiji kama Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya kujifunza kwa gharama ndogo hapa hapa nchini,” amesema Bashungwa.

Amesema kuwa ingewezekana kwenda nje ya nchi kubuni kitu ambacho tunaweza kujifunza sisi wenyewe hivyo tunajivunia suala hili na wakuu wa mikoa, makatibu Tawala na wakurugenzi nimewaomba mje hapa ili kutafsiri kwa vitendo kwenye ngazi za mikoa maana yapo mambo makubwa tunaweza kufanya, hivyo tumieni matamko ya viongozi na maono yao kufanya haya,”

Waziri Bashungwa amewataka viongozi hao kupeleka elimu waliyojifunza kwenye soko hilo kwenye maeneo yao na kuhakikisha wanawashirikisha machinga kwenye ujenzi wa miradi hiyo ambayo itatekelezwa kwenye mikoa yenye hadhi ya majiji nchini.

Kwa upande wake, Msanifu mshauri wa mradi huo, Dkt. Ibrahim Msuya amesema  soko hilo litaweza  kubeba machinga 3000 na vizimba vya aina 9 za biashara tofauti tofauti.

Amefafanua kuwa kwa sasa wanafanya usajili wa machinga kwa mfumo wa kidigitali kutokana na kujitokeza kwa changamoto ya baadhi kujisajili mara mbili jambo ambalo lilileta taswira mbaya.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohamed Builders Limited, Taher Mustafa alimshukuru Rais Samia kwa historia aliyoipa kampuni hiyo kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya serikali huku akiahidi kutekeleza kwa wakati.

“Namshukuru Rais Samia na uongozi wa jiji la Dodoma na maeneo mengine kwa kutuamini kampuni yetu na namhakikishia kuwa tutamaliza mradi kwa muda uliopangwa na kwa viwango ili izidi kutuamini na kutupa miradi zaidi,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera alisema wamejifunza kupitia mradi huo na kuahidi kuwa kwenye maeneo yao watazingatia kuwa dhamira ya Rais kuwawekea mazingira rafiki machinga linazingatiwa.

“Tunaomba kufanyia marekebisho kwenye bajeti zetu ili kuweka mpango huu hususani kwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2022/23,” amesema Homera.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.