Na Getruda Shomi, Dodoma
NAIBU Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Emmanuel Chibago ametoa pongezi kwa watumishi wa Halmashauri hiyo walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Wakurugenzi katika Halmashauri ya Wilaya Njombe Mkoa wa Njombe na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambaye ameteuliwa tena kuendelea kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji hilo, ambapo amesema kuwa hiyo ni ishara kwamba Jiji hilo lina watumishi makini na hodari.
Watumishi walioteuliwa kuwa Wakurugenzu kutoka katika menejimenti ya Jiji hilo kwa mara ya kwanza ni Sharifa Nabalang’anya aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Shabani Juma aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Ametoa pongezi hizo kwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo Agosti 4, 2021 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Chuo cha Mipango ikiwa ni kikao cha robo ya mwisho ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021 ambapo Baraza hilo lilijadili na kupitisha taaarifa za maendeleo katika Halmashauri hiyo.
“Tunatoa pongezi kwa watumishi wetu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambao wameteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri katika Mkoa wa Katavi na Njombe, tunawapongeza sana na tunajivunia kama Baraza la madiwani.” alisema Chibago.
Aidha, wateule hao watatu walipata nafasi ya kuzungumza katika kikao hicho na kutoa shukrani zao kwa wajumbe, menejimenti, na wote walioshirikiana nao katika kazi kwa nyakati tofauti.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.