NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetenga Sh Bilioni 1.7 hadi kufikia Februari 2024 kiasi cha Sh Bilioni 1.15 kimekwishatolewa kwa ajili ya kulipa posho za Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mtaa.
Ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay aliyehoji ni liji Serikali itawalipa posho Wenyeviti wa Vitongojo, Vijiji na kuongeza posho za madiwani ili kuwasaidia kutekeleza majukumu kikamilifu.
Amesema Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi ambapo imeendelea kulipa posho za viongozi hao ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.
“Katika mwaka wa fedha wa 2023/24 Serikali imetenga kiasi cha Sh Bilioni 20.8 kwa ajili ya kulipa posho za madiwani katika Halmashauri 168 ambapo hadi kufikia Februari 2024 kiasi cha Sh Bilioni 13.5 kimekwishatolewa kwa ajili ya posho za madiwani hao,” Amesema Dkt. Dugange
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.