NAIBU Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amesema Serikali imetenga fedha shilingi bilioni 16.5 kufanya ukarabati wa hospitali 19 katika mwaka wa fedha 2022/23.
Alisema hayo Bungeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge Viti Maalum, Esther Midimi aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa kuwa Hospitali iliyopo ina hadhi ya Kituo cha Afya na haikidhi mahitaji.
Dkt. Dugange alisema Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ni miongoni mwa hospitali kongwe 50, ilianza kutoa huduma kwa ngazi ya Kituo cha Afya ambapo mwaka 1989 ilipandishwa hadhi na kuwa hospitali.
Aidha, Dkt. Dugange alisema katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali itatenga fedha za ukarabati wa hospitali 31 zilizobakia ikiwemo hospitali ya Wilaya ya Meatu.
Dkt. Dugange amesema Serikali imeshafanya tathmini ya hospitali chakavu zote nchini na itaanza kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa hospitali hizo katika mwaka wa fedha ujao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.