MWANAFUNZI Luck Magashi wa Shule ya Wasichana ya Huruma iliyopo Jijini Dodoma ameingia kwenye orodha ya wanafuzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2019.
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) nchini Tanzania likitangaza matokeo kidato cha nne 2019 limeonyesha watahiniwa 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa 422,722 wamefaulu mitihani yao.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji Dkt. Charles Msonde alisema watahiniwa hao ni sawa na ongezeko la asilimia 1.38 ikilinganishwa na watahiniwa 284,126 sawa na asilimia 79.27 waliofaulu mtihani huo mwaka 2018.
Katika matokeo hayo, Dk Msonde alitaja wanafunzi 10 bora kitaifa ambapo kati yao sita wanatoka Shule ya Sekondari Francis Girls ya jijini Mbeya na miongoni mwao ni mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Huruma iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Wanafunzi hao 10 ni:-
1. Joan Ritte (St Francis Girls- Mbeya)
2. Denis Kinyange (Nyengezi Seminary- Mwanza)
3. Erick Mutasingwa (Sengerema Seminary- Mwanza)
4. Rosalia Mwidege (St Francis Girls-Mbeya)
5. Domina Wamara (St Francis Girls-Mbeya)
6. Mvano Cobangoh (Feza Boy’s- Dar es Salaam)
7. Agatha Mlelwa (St Francis Girls- Mbeya)
8. Sarah Kaduma (St Francis Girls –Mbeya
9. Shammah Kiunsi (St Francis Girls – Mbeya)
10. Luck Magashi (Huruma Girls- Dodoma)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.