• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Bunge laahirishwa hadi Januari 28, 2020

Imewekwa tarehe: November 16th, 2019

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeahirishwa hadi tarehe 28 Januari, 2020. Bunge limeahirishwa baada ya kumalizika kwa Mkutano wake wa Kumi na Saba uliofanyika tarehe 05 hadi 15 Novemba, 2019 Jijini Dodoma.

Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge ulishuhudia mabadiliko makubwa ya matumizi ya Mtandao katika kuendesha shughuli za Bunge hii ikiwa ni baada ya Waheshimiwa Wabunge kupewa 'tablets' kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

Pamoja na shughuli nyingine za Kibunge, Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge ulikuwa mahususi kwa Bunge kukaa kama Kamati ya Mipango kwa takribani siku Tano (5) kujadili na kuishauri Serikali kuhusu mapendekezo ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali wa Mwaka 2020/2021.

Aidha, katika mkutano wa Kumi na Saba, Bunge pia lilijadili na kupitisha Muswada ya Sheria ya marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 7) ya mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 7) Bill, 2019] mara baada ya kusomwa kwa hatua zote Tatu.

Mbali na hayo, Bunge pia katika Mkutano wake wa Kumi na Saba wa Bunge, lilijadili na kuridhia Maazimio saba ya Kimataifa pamoja na Azimio la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa utendaji uliotukuka kwa kipindi cha miaka minne ya Uongozi wake na pia Azimio la kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Y. Ndugai, kwa uamuzi wake wa kulifanya Bunge kutekeleza kwa vitendo dhana ya Bunge Mtandao (e-Parliament).

Akitoa Hotuba ya Kuahirisha Bunge, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alisema Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020/2021 umelenga kutekeleza maeneo ya kipaumbele ikiwa ni pamoja na kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwa kuweka mkazo katika upatikanaji wa huduma bora za jamii ikiwemo elimu, maji, afya, umeme na barabara.

Mhe. Majaliwa aliongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta zinazogusa wananchi moja kwa moja na kuhakikisha kuwa matunda ya kukua kwa uchumi yanawafikia wananchi.

Aidha, amewaasa Watanzania kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, katika kipindi hiki ambacho amekuwa akichukua hatua za makusudi kuhakikisha anajenga uchumi imara, kuboresha kipato na hali ya maisha ya wananchi.

Chanzo: www.bunge.go.tz


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.