• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Buriani Mzee B.W. Mkapa

Imewekwa tarehe: July 29th, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2020 amewaongoza Watanzania katika mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa aliyezikwa kijijini kwake Lupaso Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.

Mazishi ya Mhe. Benjamin William Mkapa yamefanyika kwa taratibu za kidini na heshima zote za kijeshi ambapo Ibada ya Mazishi imeongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga (Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limefanya gwaride la mazishi likiambatana na kupiga mizinga 21 kwa heshima ya Rais Mstaafu na Amiri Jeshi Mkuu wa Awamu ya Tatu.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria mazishi hayo wakiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na kuongoza Ibada ya mazishi, Askofu Mkuu Nyaisonga amesoma salamu za rambirambi za Baba Mtakatifu (Papa Francis) aliyewapa pole Watanzania wote na kuwataka kuwa wavumilivu na wenye matumaini na salamu za Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi na Rais Mstaafu wa Nchi hiyo Mhe. Joaquim Chissano zimesomwa na Balozi wa Msumbiji nchini Mhe. Monica Patricio Clemente.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amesema Wananchi wa Zanzibar wanaungana na Watanzania wenzao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na kiongozi shupavu na hodari aliyetoa mchango mkubwa kwa Taifa na katika kuuhifadhi na kuutunza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kwamba Wazanzibar daima watamkumbuka na kuuenzi mchango huo.

Marais Wastaafu Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wamemuelezea Hayati Benjamin William Mkapa kuwa alikuwa kiongozi hodari, mbunifu, aliyechukia umasikini na aliyeelekeza nguvu zake kujenga uchumi.

Wamempa pole Mhe. Rais Magufuli na familia ya Hayati Benjamin William Mkapa ikiongozwa na Mjane wake Mama Anna Mkapa kwa kuguswa zaidi na msiba huu mkubwa na wamewataka Watanzania wote waendelee kumuombea.

Katika salamu zake, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Watanzania kwa uvumilivu wao katika kipindi chote cha maombolezo, ameishukuru kamati ya maombolezo iliyoongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na amewashukuru viongozi wote wa Dini ambao walimlea tangu alipobatizwa na hata alipofariki dunia wamemjombea na kufanyia Ibada ya maziko.

Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kujifunza kutoka kwa Hayati Benjamin William Mkapa aliyewapenda Watanzania kwa dhati na aliyewapenda wanakijiji wenzake wa Lupaso kwani wakati wa uhai wake alipoulizwa azikwe wapi atakapofariki dunia alisema anataka azikwe kijiji cha Lupaso na sio Dodoma ambako kulikuwa na mapendekezo ya viongozi wakuu wa kitaifa kuzikwa makao makuu ya nchi.

Amewataka Watanzania wote waendelee kumuombea Hayati Benjamin William Mkapa apumzike kwa amani, na wamuombee Mama Mkapa na familia nzima ili waendelee kuwa wavumilivu na wastahimilivu baada ya kuondokewa na mpendwa wao.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa alifariki dunia tarehe 23 Julai, 2020 majira ya saa 3:30 usiku baada ya moyo wake kusimama ghafla (Cardiac Arrest) akiwa hospitali Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Taarifa kwa Umma (Idara ya mawasiliano ya Rais Ikulu)

Rais Mhe. Dkt. John Magufuli akiwa pamoja na Mjane wa Mzee Mkapa, Mama Anna Mkapa na wanafamilia wa hayati Mzee Benjamin Mkapa wakati wa shughuli ya mazishi ikiendelea.












Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.