KAIMU Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Willium Mwegoha amewaalika wawekezaji kuchangamkia fursa za uwekezaji katika shughuli anuai za chuo hicho kwa miradi inayoweza kutekelezwa kwa ubia.
Ameyasema hayo leo Desemba 17,2022 alipokuwa akizungumza kwenye Mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Mikutano Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Amesema Chuo hicho kina fursa za uwekezaji kwa ubia ikiwemo ujenzi wa hosteli za wanachuo, ujenzi wa maeneo ya biashara, michezo na burudani. "Kwa mfano Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Tegeta bado kinahitaji Mabweni kwa ajili ya wanachuo hivyo tunawaalika wawekezaji walio tayari kushirikiana nasi."
Akifafanua zaidi amesema Chuo Kikuu cha Mzumbe kina sera ya uwekezaji ya mwaka 2020 inayotoa fursa ya ubia na wawekezaji mbalimbali.
Katika hafla ya mahafali hayo ya 21 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewatunuku Shahada za Umahili wahitimu 240 katika fani mbalimbali.Idadi ya wahitimu wanawake inayoendelea kuongezeka kila mwaka ni 114 sawa na asilimia 47.5 huku wanaume wakiwa ni 126 sawa na asilimia 52.5.
Wahitimu 89 wametunukiwa Shahada ya Umahili ya Biashara katika Menejementi ya Mashirika, wahitimu 45 Shahada ya Umahili ya utawala wa Umma, Shahada ya umahiri ya Sayansi katika Menejiment Rasilimali watu wanamahafali 24, Shahada ya Umahiri ya Sayansi katika Uhasibu na Fedha 7 na Shahada ya umahiri ya Sayansi katika Menajimenti ya Ununuzi na Ugavi wakiwa 14.
Wengine ni Shahada ya umahiri ya Sayansi katika menejimenti ya Masoko 6, Shahada ya umahiri ya Biashara katika Menejimenti ya Mashirika, Watendaji Wakuu 13, Shahada ya umahiri ya Sayansi Katika Uchumi Tumizi na Biashara 14, Shahada ya Umahiri ya Utawala wa umma-Watendaji Wakuu 6 pamoja na Shahada ya Umahiri ya Uongozi na Manajimenti wahitimu 13.
Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Saida Yahya-Othman akizungumza na wahitimu, amewataka kutumia elimu walioipata kutatua changamoto mbalimbali huko waendako.Amesema elimu waliyoipata inatakiwa iwe imetufungua siyo tu kiuchumi ili tupate ajira, bali pia kisiasa kwa ajili ya kujua haki zao na kijamii isaidie kulinda jamii na tamaduni na kuzitetea.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.