• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

CMT Jiji la Dodoma yapongezwa ukusanyaji mapato

Imewekwa tarehe: June 17th, 2022

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

TIMU ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma (CMT) imepongezwa kwa kazi nzuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na kukumbushwa kusimamia taratibu za utumishi ili kuwa na mafanikio.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatuma Mganga alipokuwa akiongea na Timu ya Menejimbenti (CMT) ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa jiji hilo leo.

Dkt. Mganga alisema “niwapongeze CMT yenu kwa ukusanyaji mzuri wa mapato. Nyie si watumishi tu, bali ni viongozi. Kupata neema ya uongozi si masihara. Wakuu wa idara mnatakiwa kumsaidia Mkurugenzi kutekeleza majukumu yake kwa kusimamia taratibu na sheria za utumishi wa umma”.

Aidha, amewataka wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kufanya vikao vya kazi wa wafanyakazi walio chini yao ili kujadili utendaji kazi. Ametoa mfano kwa kusema “Ni vizuri migao ya fedha za matumizi ya kawaida ziwekwe wazi kwa watumishi wote na siyo viongozi kugawa wenyewe bila wafanyakazi waliochini yenu kuwa na taarifa. Uwazi wa kushirikishana katika utendaji kazi huwa unasaidia kupata usaidizi wa mawazo na kuyasimamia. Tubadilike katika eneo hili, kila mmoja apangiwe kazi kwa uwazi na kupimwa utendaji wake na kupongezwa utekelezaji wake” alisema Dkt. Mganga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema kuwa lengo la CMT ya jiji hilo ni kutoa huduma bora kwa wananchi. “Sisi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wananchi wote ni wetu na tuna wajibu wa kuwahudumia. Niishukuru TAMISEMI na Ofisi yako kwa kutupatia watumishi wazuri. Mimi kwenye timu yangu sioni mtumishi ambae ni mzigo. Ndugu Katibu Tawala Mkoa nikuhakikishie kuwa ndani ya miezi michache utaona matokeo ya kazi. Tunayo magari ya kutosha na tumeagiza mitambo ambayo itaingia mwezi Julai, kwa hiyo kazi zetu tutazitekeleza ipasavyo. Tunataka tabia hii ya utendaji wa kazi wa CMT tuihamishie kwa wafanyakazi walio chini yetu” alisema Mkurugenzi Mafuru.

Katibu Tawala Mkoa amefanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuongea na CMT na Wafanyakazi kwa nyakati tofauti ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza tarehe 16-23 Juni, 2022.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.