• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Corona, hadi sasa hatuna maambukizi ya ndani kwa ndani, mgonjwa wa kwanza amepona - Waziri Ummy

Imewekwa tarehe: March 26th, 2020

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, amebainisha kuwa, hadi sasa Tanzania imeweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani ya ugonjwa (COVID-19) na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga.

Amesema, wasafiri 245 walioingia Tanzania Bara na Zanzibar tangu Machi 23, mwaka huu, wametengwa kwenye hoteli na maeneo yaliyoandaliwa na Serikali kwa gharama zao.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Corona nchini.

Amesema hadi sasa hakuna maambukizi ya ndani (Local transmission) na wagonjwa 13 waliothibitika kuwa na virusi vya ugonjwa huo wanaendelea vizuri.

“Hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa lengo lakutimiza dhamira nzuri ya serikali ya kupunguza hatari ya kusambaa kwa haraka maradhi haya nchini, tunashukuru Mungu bado hatuna ‘Local transmission,” amesema.

Aidha, amesema mgonjwa wa kwanza wa Arusha, amepona Corona na taratibu za kumruhusu kurudi nyumbani zinaendelea.

“Mgonjwa wetu amepona COVID19 na amepimwa mara tatu hana, tumeanza utaratibu wa kumrudisha nyumbani, kazi ambayo nimemuelekeza Katibu Mkuu aifanye sasa hivi suala la kutoa elimu ili kuondoa unyanyapaa, kulaumiana na kunyoshewa vidole Isabela,” amesema.

Kadhalika, amesema wasafiri hao 245 wamewekwa karantini kwa siku 14 kwenye maeneo maalum ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Dkt.John Pombe Magufuli.

“Tangu agizo la Rais wasafiri 111 kwa Tanzania barana 134 kwa Zanzibar wametengwa kwenye hayo maeneo, na tunasisitiza mikoa yote nchini kuendelea na zoezi la kubainisha sehemu zitakazo tumika kuweka wasafiri bila kuleta usumbufu usio wa lazima,” amesema Waziri Ummy.

Pamoja na hayo, Waziri huyo amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Zanzibar imeendelea kufanya ukaguzi kwa kupima joto la mwili kwa wasafiri wote wanaoingia nchini.

“Kuanzia Januari mosi mwaka huu hadi sasa wasafiri 1,890,532 wamefanyiwa ukaguzi wa kupimwa joto kwenye vituo 27 vya mipakani ikiwemo viwanja vya ndege na bandarini na kwa saa 24 zilizopita jumla yawasafiri 3,471 wamefanyiwa ‘screening’,” amesema.

Amefafanua kuwa watu 273 wamepimwa sampuli za kupima virusi vya Corona katika Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii hadi Machi 26, 2020.

“Kati ya sampuli hizo zilizopimwa 260 hazikuonesha uwepo wa virusi hivyo na sampuli 13 zilithibitika kuwa na virusi, wagonjwa hawa ni kutoka Mkoa wa Arusha (2), Dar es salaam(8), Zanzibar (2) na Kagera (1),” amesema Ummy.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo ameshukuru msaada wa vifaa mbali mbali ikiwemo vya kupima virusi haraka (Rapid test kits) kutoka kwa Taasisi zilizopo Jamhuri ya watu wa China za Jack Ma na Alibaba na vitasambazwa kwenye hospitali zilizotengwa maalum kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa hao.

Waziri Ummy amesema maabara iliyopo haijazidiwa na utaratibu mzuri umeandaliwa wa upimaji wa sampuli kutoka mikoani.

Aidha, amesema serikali inatarajia kuongeza maabara sita na Zanzibar moja.

“Tumeona pia kuna haja ya kuongeza maabara, tayari maabara ya Chuo Kikuu Sokoine (SUA) inaweza kupima sampuli, pia maabara za NIMR Mbeya, Tanga, Mwanza na Arusha ile maabara ya St. Nelson Mandela, hili tumeliona lakini tumeona kuna haja ya kuwa na ‘rapid test’, tupo vizuri hatujazidiwa na sampuli zinafika kwa wakati kwenye maabara yetu,” ameongeza kusema.

Waziri huyo amesema vipimo vya kupima virusi kwa haraka vitawekwa kwenye Hospitali za Mikoa, Kanda na kwenye mipaka.

“Jumuia ya Afrika Mashariki pia jana tumepata msaada wa maabara zinazotembea, na tutapata mbili kwa Tanzania ambazo zitapelekwa Arusha na Zanzibar,” amesisitiza.

Naye, Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed, amewataka Watanzania kujikinga na ugonjwa huo huku akisisitiza kuwa Serikali haina nia ya kumuweka mtu kambini kumtesa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na Naibu Katibu Mkuu wake wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Chanzo: afyablog.moh.go.tz

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.