• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

DC Shekimweri ahimiza usafi kudhibiti magonjwa Dodoma

Imewekwa tarehe: January 24th, 2025

Na. Shahanazi Subeti, DODOMA

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri aliitaka jamii kuzingatia suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kujikinga na magonjwa na kufanya mji kuwa safi na salama katika kipindi hiki cha maandalizi ya bajeti ya halmashauri ili wananchi wawe na afya bora.

Aliyasema hayo katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kupokea na kujadili mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2025/2026.

Alhaji Shekimweri alisema “wenzetu maafisa afya, watendaji wa kata, changamoto za uchafu wa mji wetu ni usimamizi kwa sehemu fulani, yapo maeneo ya kampuni za usafi, yapo maeneo yanavikundi vya usafi, lakini ni wajibu wa mwananchi mmoja mmoja kufanya usafi wa eneo lake. Kwahiyo, tuimarishe usimamizi, na kuna makampuni na vikundi na vinalipwa kwa kufanya kazi hizo”.

Akiongelea suala la usalama katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa kamera za usalama (CCTV) ni muhimu katika kuimarisha usalama. “Tunachokimaanisha tunapoelekea utaona askari wachache barabarani wanapita kwenye doria, kwasababu kutakuwa na Kamera zinazofanya kazi, badala ya kutuma askari, watakuwa wanaona tukio, lakini katika baadhi ya maeneo ya “observation points” watakaa na pikipiki zao ili kukamata watu wanaofanya matukio ya wizi. Tunataka tuelekee katika mazingira ambayo hakuna ‘panyaroad’ Dodoma, kwasababu muda wote mji unaangaliwa na mitambo ya kisasa kupitia Jeshi la Polisi na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama” alisema Alhaj Shekimweri.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma alisema kuwa amepokea mchango unaohusu mkakati wa dharura na majanga.  “Mfano jana kulikuwa na tukio la moto, wengi mmeona fremu takribani 12 na stoo mbili ziliungua kwa moto lakini tukabaini Jiji letu lina 'fire hydrant’ (mitambo ya kuunganisha kwa ajili ya kuzimia moto) 74 mji mzima, lakini ambazo zinafanya kazi hazizidi 40. Kwahiyo, Jiji limepokea hiyo rai kwa haraka kulisaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwasababu wananchi ni wa halmashauri. Hivyo, ni wa kamati hii ya ushauri wa maendeleo ya wilaya na ndio walipa kodi. Kwahiyo, ni jambo la wananchi wetu tufanye huduma ya mitambo hiyo” alisema Alhaj Shekimweri.

Aliwataarifu wajumbe kuwa bajeti ya halmashauri inategemea ukusanyaji wa kodi na kuwataka kudai risiti kwa kila malipo wanayofanya. “Ndugu zangu wafanyabiashara, wanataka kuongeza faida, anaweza kukuuzia na asikupatie risiti yeye atapata faida lakini wewe utakuwa umeidhulumu serikali na umejidhulumu wewe mwenyewe. Maendeleo yote haya hayawezi kufanyika kama haukusanyi kodi” alisema Alhaj Shekimweri.

Nae, Katibu wa AAFP, Zuhura Mganga, aliishauri serikali kuhusu Soko la wazi la Machinga kufungwe CCTV kamera za kutosha ili kuzuia vitendo vya wizi. “Nashauri kuhusu usalama wa Soko la wazi la Machinga pale kumekuwa na wizi, hakuna kamera za kutosha na hata kamera zilizopo hazioneshi pande zote” alisema Mganga.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu Bakwata, Kakongwe Misambano, alichangia katika suala la afya na usalama barabarani. “Kwa upande wa afya, ukiangalia tunaongelea bajeti sana lakini utendaji wake unakuwa hauko sahihi. Mfano, mitaro ya barabara ya Nkuhungu ambayo imetengenezwa kwa ajili ya bwawa, na linahamisha watu kila mwaka wakati wa mvua, usalama kwa watoto hakuna kwasababau maji hayaendi badala yake yanatuwama. Kwahiyo, …bajeti ambazo zinatengwa zinafanya nini?. Kwasababu, hiyo mitaro inarudisha nyuma, badala ya kupeleka mbele ili maji yaishe” alisema Misambano

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.