MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Josephat Maganga, leo tarehe 09 Disemba, 2020 tukiadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika ameshiriki na kukagua shughuli za usafi wa mazingira na uondoshaji wa taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma.
Katika ukaguzi huo Maganga alisisitiza Jiji la Dodoma kuhakikisha linaondosha taka ngumu katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu kwa wakati hasa katika kipindi hiki cha mvua pamoja kuagiza makampuni na vikundi vinanyojihusisha na shuguli za usafi wa mazingira kuboresha vifaa kinga na vitendea kazi kwa wafanyakazi wao.
"Jiji la Dodoma linakua kwa kasi sana hivyo tunatakiwa sana kuzingatia usafi hasa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi kama vile sokoni na vituo vya mabasi, pia niwaagize wamiliki wa makampuni na vikundi vinavyoshughulika na usafi hapa Jijini kuhakikisha mnawawekea wafanyakazi wenu mazingira wezeshi ya kufanyia kazi kama kuwapatia vifaa kinga na vitendea kazi bora ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi zaidi." Alisema Maganga.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.