• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Dhahabu kuanza kusafishwa Dodoma, BoT kuinunua

Imewekwa tarehe: August 22nd, 2019

Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa na kiwanda cha kuchenjua na kusafisha dhahabu kinachotarajiwa kuanza kazi Oktoba mwaka huu.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Madini, Doto Biteko baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kitakachochenjua na kusafisha dhahabu kwa asilimia 99.9.

Amesema mbali na kusaidia wafanyabiashara nchini katika kuchenjua na kusafisha dhahabu zao, pia uwepo wa kiwanda hicho utawezesha nchi kuwa na akiba ya madini hayo yatakayonunuliwa na Benki ya Kuu (BoT).

Januari mwaka huu, Rais John Magufuli aliagiza BoT kuwa na akiba ya dhahabu na kuhimiza haja ya serikali kudhibiti usafirishaji wa madini kutoka hapa nchini ambayo ni nchi ya nne kwa kuzalisha dhahabu.

“Tunatakiwa kuanza kununua dhahabu, BoT inatakiwa kuwekeza kwenye hili. Tunatakiwa kuwa na akiba yetu si tu kwenye dola bali hata kwenye dhahabu, kwa sababu dhahabu ni fedha,” amesema Rais Magufuli.

Biteko amesema kuanzia Oktoba mwaka huu, BoT itaanza kununua dhahabu iliyosafishwa ambayo itaweka kwenye “akiba ya Taifa ya dhahabu’ na hatimaye kusaidia nchi kuuza dhahabu na kushindana kwenye soko la kimataifa.

Amesema hatua ya kuanzisha kiwanda cha kuchenjua na kusafisha dhahabu nchini ni takwa la kisheria kutokana na mabadiliko ya hivi karibuni ya Sheria ya Madini, na kuongeza kuwa mpaka sasa tayari serikali imetoa leseni mbili za kuanzisha kiwanda cha kusafisha dhahabu mkoani Dodoma na Mwanza.

Amesema walijitokeza jumla ya waombaji 24 na waliopewa vibali wa uendeshaji wa shughuli za kurefine na ku-smelte ni sita.

“Kati ya viwanda hivyo sita vitakavyojengwa nchini, viwanda viwili ni vya kurefine madini ya dhahabu, copper na silver ambavyo vipo katika mikoa ya Dodoma na Geita,” amesema na kuongeza kuwa viwanda vinne vya Smelter vimejengwa Kyerwa mkoani Kagera, Mpwapwa (Dodoma) na Kahama (Shinyanga).

Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Ferenc Milnar alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho uliogharimu dola za Marekani milioni 2, umekamilika kwa asilimia 75 na kwamba hivi sasa wanasubiri vifaa kutoka nchini Italia.

Alisema baada ya kufika vifaa hivyo nchini mwezi ujao, watatumia siku saba kuvifunga. Molnar pia alimuhakikishia waziri kuwa watahakikisha ujenzi wa kiwanda hicho unakamilika ndani ya muda uliopangwa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha hicho, Prince Mugisha alisema wataanza kwa usafishaji wa mfano ambao utakuwa kilo 30 hadi 50 kwa siku. Aliongeza kuwa mwakani watakuwa wakisafisha kilo 1,000 kwa siku.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema utekelezaji wa sehemu wa Sheria ya Madini inayotaka theluthi moja ya mrahaba utolewe kama dhahabu utaanza kutekelezwa mara baada ya kiwanda cha uchenjuaji wa dhahabu cha kwanza kukamilika mwezi Oktoba.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge aliwahakikisha wawekezaji wanaotaka kuwekeza mkoani Dodoma kuwa watapata msaada unaotakiwa na kuwakaribisha kufika ofisini kwake kama wanakumbana na urasimu wa aina yoyote.

Chanzo: HabariLeo Online



Matangazo

  • TANGAZO LA MABADILIKO YA TAREHE YA USAHILI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA WASIMAMIZI JIMBO LA MTUMBA October 03, 2025
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA- DODOMA MJINI October 03, 2025
  • TANGAZO LA MAJINA YA MAKARANI WAOGOZAJI WAPIGA KURA October 03, 2025
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Rc Senyamule awasihi wawekezaji sekta binafsi kuwekeza Dodoma

    October 03, 2025
  • CCTV kamera mwarobaini wa wavunjifu wa sheria jiji la Dodoma

    October 02, 2025
  • Wadau wa afya wapongezwa kwa juhudi zakudhibiti vifo vya wajawazito

    October 01, 2025
  • UONGOZI WA KLABU YA MICHEZO OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAKUTANA NA RAS KAZUNGU

    September 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.