Na. Emmanuel Lucas, CHANG’OMBE
Diwani wa Kata ya Chang`ombe, Bakari Fundikira amewataka wananchi kuendelea kutunza amani, upendo na mshikamano hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa kutoa tamko la uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kauli hiyo aliitoa kwa waandishi wa Habari baada ya kikao na viongozi wa Soko la Mavunde kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Kata ya Chang'ombe iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Diwani Fundikira alisema “kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Waziri mwenye dhamana Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa ameshatoa tarehe ya uchaguzi ambayo itakuwa tarehe 27 Novemba, 2024. Rai yangu kwa wananchi wa Kata ya Chang`ombe na wananchi wengine, itakapofika wakati wa uandaaji wa daftari la wapiga kura cha kwanza tujitokeze wananchi wote wenye sifa tujiandikishe ili tuwe na sifa ya kuchagua na kuchaguliwa”.
“Kimsingi kwenye suala la ulinzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, sisi katika kata kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwasababu kuna Polisi Kata, tunakamati ya ulinzi ya kata lakini pia tunazidi kutoa elimu kwenye ngazi za mitaa kuhusiana na suala la kutunza amani, upendo na mshikamano” aliongeza Fundikira.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.