• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Dkt. Abbasi akabidhi Idara ya Habari, asifu uamuzi wa Rais Samia

Imewekwa tarehe: October 18th, 2021

KATIBU MKUU wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo. Dkt Hassan Abbasi   leo Oktoba 18, 2021 amekabidhi rasmi Idara ya Habari MAELEZO na Sekta ya Habari kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Dkt, Zainabu Chaula huku akipongeza uamuzi huo alioufanya Rais Samia Suluhu Hassan ambao ameuelezea kuwa ni uamuzi muhimu na wa kimkakati wa kuboresha sekta zote kwa maslahi mapana ya Taifa.

Dkt. Abbasi ambaye ameilea sekta hiyo kwa miaka mitano na miezi miwili na siku 9 amesema maamuzi hayo yamekuja wakati mwafaka na kusisitiza kuwa sekta hizo zimewekwa mahali panapotakiwa na kwamba ufanisi kwenye sekta hizo utaongezeka na kuleta mafanikio makubwa tofauti na awali.

Amewataka wataalam na waandishi wa habari kote nchini kuzingatia misingi ya taaluma ya habari na kanuni kuu za maadili ambazo amezitaja kuwa ni ukweli, usahihi na umakini ili kusaidia na kuchangia maendeleo ya nchi.

“Ndugu zangu napenda kuwasihi na kuwaambia Uandishi wa Habari ni taaluma hivyo kuweni na wivu na kulinda taaluma yenu kwa kutimiza haki na wajibu wenu, ni vema mkazingatia taratibu za uandishi kuna mambo ambayo mnaruhusiwa kisheria na mambo ambayo yanakatazwa na sheria za nchi basi ni muhimu sana kuzingatia.” ameongeza Dkt. Abbasi.

Aidha, ameishukuru Serikali kwa kumpa nafasi ya kutoa mchango wake kwa Sekta na Idara ya Habari na ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati wakati wowote ambapo kwa sasa anabaki kuwa mtaalamu na mdau wa sekta hiyo.

Akifafanua baadhi ya mambo aliyokabidhi, amesema amekabidhi ofisi ikiwa na watumishi 37, magari manne pamoja na Sheria  ya Huduma za  Habari na Kanuni zake ambayo ndiyo mwongozo mkuu kwenye sekta hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainabu Chaula amempongeza Dkt. Abbasi kwa kazi kubwa aliyofanya kwenye sekta hiyo na amemhakikishia kuendelea kufanya kazi za taaluma ya habari kwa uadilifu.

“Nikupongeze sana kaka yangu Dkt. Abbasi tumefanya kazi kwa karibu, tunategemeana na tutaendelea kuboresha pale tulipoacha” ameongeza Dkt. Chaula.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Idara ya Habari- MAELEZO kwa Makatibu Wakuu hao, Mkurugenzi wa Idara hiyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amemshukuru Mhe. Rais kwa uamuzi huo na kumpongeza Dkt. Abbasi kwa mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika kipindi chote alichokuwa akiilea sekta hiyo.

“Niseme wazi ndugu zangu nampongeza sana Dkt. Abbasi amefanya kazi kubwa sana kwenye sekta hii na kuiheshimisha taaluma hii hapa nchini”. Amefafanua Msigwa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.