• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Dkt. Sagamiko asema, ugawaji jimbo hauna athari kwa huduma zinazotolewa na Jiji la Dodoma

Imewekwa tarehe: March 23rd, 2025

Na, Nancy Kivuyo, DODOMA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alitoa hofu Baraza la Madiwani kuwa kukidhi vigezo vya ugawaji wa Jimbo la Dodoma Mjini hauna athari katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika kuwahudumia wananchi.

Aliyasema hayo wakati akijibu hoja za madiwani waliohudhuria katika Mkutano maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa ya mapendekezo ya mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. 

“Mgawanyo wa jimbo kwa upande wa tarafa hauna kikwazo chochote, kama ni kata ni kikwazo kwasababu kata moja haiwezi kuwa katika majimbo mawili. Leo tutaangalia zaidi kwenye kata” alisema Dkt. Sagamiko.

Aliongeza kuwa, athari za mgawanyo wa jimbo kimapato unalenga mgawanyo wa majimbo na sio shughuli za kiutendaji. “Niwatoe wasiwasi, utoaji wa huduma kwa wananchi utaendelea kama ilivyokua awali na Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Baraza litakua moja bila kujali jimbo analotoka diwani. Mipango itapangwa kulingana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma” alimalizia Dkt. Sagamiko.

Nae, Diwani wa Kata ya Ihumwa, Edward Magawa, aliishukuru serikali kwa kuleta mapendekezo ya mgawanyo wa Jimbo la Dodoma Mjini kwakuwa jiografia yake imekua kubwa na namna ya kuhudumia kata 41 kwa pamoja ni changamoto. “Binafsi niipongeze serikali kwa namna wameona ni vema kugawanya jimbo ili kupata urahisi wa kuhudumia wananchi. Nimpongeze pia Mheshimiwa mbunge kwa kazi nzuri, amejitahidi kuhudumia kata 41 kwa namna alivyoweza lakini sasa itakua rahisi mbunge kuwafikia wananchi na kutatua changamoto kwa urahisi” alisema Magawa.


Kwa upande mwingine, Diwani wa Viti Maalum, Wendo Kutusha alisema “taarifa hii nimeipokea kwa furaha kubwa sana kwasababu kata 41 alizokua anashughulika nazo mbunge wetu Mavunde ni nyingi mno. Kuna majimbo mengine yana kata chache sana. Kwahiyo, ujio wa mgawanyo huu utasaidia mbunge kuzifikia kata zote. Naishukuru sana Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuliona jimbo hili linafaa kuwa na wawakilishi wawili watakaoendeleza maendeleo ya Jiji la Dodoma. Matarajio yangu ni kwamba tunatarajia kuwa shughuli za maendeleo ziwe nyingi na maendeleo yakaonekane katika jamii zetu” alimalizia Kutusha. 

Mapendekezo ya kugawanya Jimbo la Dodoma Mjini lenye jumla ya wapiga kura 795,000 na kuwa majimbo mawili, Jimbo la Dodoma Mjini lenye jumla ya watu 412,000 na kata 21 na Jimbo la Mtumba lenye jumla ya watu 383,000 na kata 20 kwa lengo la kusigeza huduma kwa wananchi ambao ndio msingi wa demokrasia ya uwakilishi ndani ya Wilaya ya Dodoma yamepokelewa na kupitishwa kwa kauli moja.




Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.