• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Dodoma Jiji FC, Gari Limewaka

Imewekwa tarehe: February 17th, 2025

Na. Mussa Richard, DODOMA

Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, imeichakaza Klabu ya Soka ya Fountain Gate FC, kwa kuichapa bao Moja kwa nunge katika mchezo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara, mchezo uliopigwa katika dimba la Jamhuri hapo jana, bao pekee la Dodoma Jiji FC, liliwekwa kimiani na mchezaji Idd Kipagwile, kwa mkwaju wa penati mnamo dakika ya 37 ya mchezo.

Baada ya mchezo kutamatika Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Mecky Mexime alisema “niwapongeze wachezaji wangu kwa kupambana na kuhakikisha tunashida mchezo. Mchezo ulikua ni mgumu ukizingatia hatuna idadi ya wachezaji wengi wenye utimamu kimwili lakini wachezaji waliopo kwa uchache wao wameweza kuonesha umuhimu wao kwenye timu wamepambana kadri ya uwezo wao tumeweza kushinda mchezo, tumetengeneza nafasi kwa idadi kubwa sana kipindi cha pili lakini kutokana na presha ya mchezo tukashindwa kuzitumia lakini kwenye mchezo ujao tutajiandaa kwenda kuhakikisha tunatumia nafasi tunazotengeneza kwa usahihi”.

Akiongelea malengo ya timu alisema kuwa ni kukusanya alama kwa kila mchezo ulio mbele yao. “Ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi mwishoni mwa msimu, na ushindi huu mfululizo kwa mechi za nyumbani unatuongezea nguvu zaidi ya kupambana huku tukusubiri majeruhi wapone haraka warudi kwenye timu ili tuje tupambanie malengo yetu kwa pamoja” aliongeza Mexime.

Nae, nyota wa mchezo huo Mwanakibuta David baada ya dakika 90 kutamatika aliwashukuru wachezaji wenzake kwa kupambana kuhakikisha timu inapata matokeo chanya licha ya kukumbwa na wimbi la majeraha kwa baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu mchezo umeisha salama na tumeweza kupata alama tatu muhimu, lakini kwa ukubwa niwapongeze wachezaji wenzangu kwa kupambana kwa dakika zote mpaka tumefanikiwa kushinda mchezo wa pili mfululizo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipo washukuru mashabiki wetu ambao wamejitokeza kwa wingi kutuunga mkono, kama wachezaji tumefarijika sana na tutaendelea kujituma kuhakikisha mashabiki wanafurahi na timu inazidi kukusanya alama na kupanda katika nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi” alisema Kibuta.

Katika michezo mitatu ya mwisho Dodoma Jiji FC, imefanikiwa kukusanya alama saba kibindoni, ikitoa sale mchezo mmoja, ikishinda michezo miwili. Mchezo ujao Dodoma Jiji FC, itasafiri kuwafuata Nyuki wa Tabora, Tabora United mchezo unaotarajiwa kuchezwa katika dimba la Ali Hassan Mwinyi Februari 28 saa 10:00 jioni.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.