Timu ya Dodoma Jiji FC tayari ipo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mchezo wake wa nne wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakapopambana na wenyeji Polisi Tanzania katika uwanja wa Ushirika Moshi kesho mchezo utakaoanza majira ya saa 8 mchana.
Dodoma Jiji FC iliwasili mjini hapa ikitokea Jijini Tanga ilipocheza na Coastal Union Jumapili iliyopita na kuambulia sare yake ya kwanza baada ya kushinda michezo miwili ya mwanzo. DJFC inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikitanguliwa na KMC, Azam na Simba baada ya kujikusanyia pointi 7 katika michezo yake mitatu.
Katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, Dodoma Jiji itawakosa nahodha wake Omary Kibacha na mshambuliaji wake hatari Anuary Jabir walioumia katika mchezo wao na Coastal Union, hata hivyo habari njema ni kurudi uwanjani kwa wachezaji waliokuwa majeruhi mshambuliaji Omary Kanyoro na mlinzi wa kushoto Abubakari Ngalema.
Kocha mkuu Mbwana Makata bado ana matumaini makubwa ya kushinda mchezo na Polisi na amesema wamejipanga kusahihisha makosa ya mchezo uliopita ili wapate ushindi na kuondoka na pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania.
Kila la heri timu yetu Dodoma Jiji FC.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.