Timu ya Dodoma Jiji FC inayoongoza ligi daraja la kwanza kundi A leo imeonesha dhamira yake ya kupanda daraja ili kucheza Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kuisambaratisha timu ya Mbeya Kwanza kwa jumla ya mabao 3 - 1 katika mchezo mkali uliochezwa kwenye dimba la Jamhuri Jijini Dodoma.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na mamia ya wapenda soka wa Jiji la Dodoma ambao wamekuwa na kiu ya muda mrefu kuona timu kutoka Dodoma ikicheza ligi kuu, walishuhudia mchezaji wao Anuary Jabir akifunga magoli yote matatu (Hat trick). Miongoni mwa wapenda soka waliohudhuria mchezo huo ni pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na watu Wenye ulemavu Mhe. Anthony Mavunde, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Abbas na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.