KIKOSI cha walima Zabibu wa Makao Makuu Dodoma Jiji FC wapo katika mazoezi na maandalizi makali kukabiliana na klabu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara siku ya jumanne Novemba 15,2022 saa 10:00 jioni katika dimba la Uhuru Jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza na wanahabari katika uwanja wa mazoezi Kocha Mkuu wa Timu hiyo Melis Medo amesema kuwa wanajua kuwa hawako katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi ila Hilo haliwafanyo waingie kinyonge katika mchezo huo.
"Malengo yetu makubwa ni kushinda katika mchezo huo ili tuanze rasmi utaratibu wa kushinda katika michezo yetu yote inayofuata"
Medo aliongeza kuwa Hali ya wachezaji kwa ujumla ni nzuri na wako tayari kwaajili ya mchezo huo hivyo amewaomba mashabiki kutovunjika moyo na kuendelea kujitoa kwaajili ya timu yao kwani nyakati ngumu huwa hazidumu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya timu hiyo Moses Mpunga amewataja wachezaji ambao wataukosa mchezo huo.
"Wachezaji ambao watakosekana katika mchezo huo ni pamoja na Aboubakar Ngalema ambae bado ni majeruhi, Mwanaa kibuta na Aron Kalambo ambao wana kadi tatu za njano, ila wachezaji wengine wote wako sawa kwaajili yachezo" Alieleza Mpunga.
Klabu ya Dodoma Jiji imecheza jumla ya michezo kumi, ikishinda mchezo mmoja, ikitoa sare michezo mitatu na kupoteza michezo sita, ikijikusanyia alama sita na kushika nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.