TIMU ya Dodoma Jiji imeibuka kidedea katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021 baada ya kuwachapa ‘Wajelajela’ wa Tanzania Prisons kwa bao moja kwa sifuri bao lililofungwa na Dickson Ambundo katika dakika ya 55 ya mchezo ambao umechezwa katika dimba la Nelson Mandela Mkoani Rukwa.
Akizungumza baada ya mchezo huo Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji Mbwana Makata amewapongeza wachezaji wake kwa matokeo hayo ambayo yanawasogeza mpaka nafasi ya tano ya msimamo wa ligi hiyo.
Makata amesema kuwa licha ya mchezo huo kuwa mgumu kwa dakika zote wachezaji wake wamepata nafasi kadhaa na kushindwa kuzitumia hivyo amechukua hayo kama changamoto na atakwenda kuyafanyia kazi ili katika mchezo unaofuata waweze kufanya vizuri zaidi.
“Ulikua mchezo mgumu kwetu kutokana na aina ya mchezo ambao Prisons wanacheza lakini tuliweza kuwasoma na kujua madhaifu yao yapo wapi tukayatumia kama silaha na tukaweza kupata matokeo” alisema Makata.
Dodoma Jiji sasa wamefikisha alama 37 ambazo zimewafanya wapande kwa nasafi mbili hadi nafasi ya tano ya msimamo wa ligi Kuu Tanzania Bara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.