• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Dodoma kutoa Hati za kielektroniki kuanzia Julai Mosi

Imewekwa tarehe: June 15th, 2021

OFISI ya Ardhi mkoa wa Dodoma itaanza kutoa Hatimiliki za Ardhi za Kielektroniki kwa wamiliki wa ardhi kuanzia Julai mosi, 2021.

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma, Thadei Kabonga wakati wa utoaji hati za ardhi 223 kwa wananchi waliorasimishiwa maeneo yao kwenye mitaa ya Miganga na Chinyika katika kata ya Mkonze mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.

Kwa mujibu wa Kabonga, kwa sasa ramani zote za mkoa wa Dodoma zipo kwenye mfumo wa kidijitali hivyo ofisi yake itaanza kutoa hati za ardhi za kielektroniki kwa kuwa hati hizo ziko katika nakala laini.

Kwa sasa Wizara ya Ardhi imewekeza, imeboresha na kuongeza matumizi ya mifumo ya kidigitali ambapo tayari Hati za Kielektroniki nchini zimekuwa zikitolewa kwenye manispaa nne za mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni Ilala,Temeke, Kinondoni na halmashauri ya manispaa ya ubungo na hati hiyo ni ya kurasa moja.

"Ramani zote za dodoma kwa sasa zipo kidigitali na Julai mosi mwaka huu tunaanza kutoa hati za kieleltroni maana hati zote ziko katika nakala laini" alisema Kabonga. 

Aliwataka wakazi wa Dodoma wanaomiliki ardhi kuhakikisha wanapimiwa maeneo yao na kupata hati kwa kuwa gharama za upatikamaji hati sasa imepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma na kusisitiza kuwa lengo la ofisi yake ni wananchi katika jiji la Dodoma kupata hati zao.

Katika kuhakikisha ardhi ya jiji la Dodoma inapangwa, inapimwa na kumilikishwa, Kamishna Kabonga alisema, ofisi yake ilipeleka timu ya wataalamu katika mitaa mbalimbali ikiwemo ya Miganga na Chinyika kwa lengo la kupima maeneo hayo lakini muitikio wa wananchi umekuwa mdogo.

Naye Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde aliyekuwa mgeni rasmi kwenye zoezi la kugawa hati kwa wananchi wa mitaa ya Miganga na Chinyika alilielezea tukio la utoaji hati kwa wananchi waliorasimishiwa makazi kuwa ni tukio la kihistoria kwa kuwa hati zinawafuata wananchi katika maeneo yao badala ya wao kuzifuta.

Alisema, hatua ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika jiji la Dodoma unaofanywa na Wizara ya Ardhi  Nyumba na Maendeleo ya Makazi unalifanya jiji hilo kupimwa kwa kasi na kupunguza ongezeko la makazi holela, thamani ya ardhi kupanda sambamba na kuondoa migogoro ya ardhi.

"Leo ni furaha mji unapimwa kwa kasi unaondoa uholela, kuongezeka thamani ya ardhi pamoja na kuondoa migogoro, ukipima eneo unatatua changamoto zote na dododma ikipimika na kupangwa vizuri inakuwa sura ya makao makuu" alisema Mavunde.

Mavunde aliwaeleza wananchi wa mitaa ya Miganga na Chinyika kuwa hati waliyopewa inawapa uhakika wa miliki pamoja na hati hiyo kutumika na taasisis za kutoa mikopo kwa wananchi.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji wa halmashauri ya jiji la Dodoma William Alfayo alisema, kazi ya upangaji na upimaji iliyofanyika kwenye mitaa miwili ya Miganga na Chinyika mkoani Dodoma ni sehemu ya kazi inayofanyika kwenye kata zote za jiji la Dodoma na zoezi hilo linafanyika kwa mujinbu wa mpango kabambe wa jiji la Dodoma 2019 hadi 2039. 

"Tusisahau kilimo cha zabibu katika mipango yetu, sisi tunaendelea  na upangaji na upimaji wa mashamba ya zabibu katika maeneo ya Mjini na ninatoa wito kwa wana Dodoma kuzingatia uwekezaji katika zao la zabibu ikiwemo uchakataji wa zao hilo" alisema Alfayo.

 

 

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.