WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi maalumu Mhe. Dorothy Gwajima, amefanya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule pamoja Makatibu wa Wizara saba zinazishiriki kwenye maandalizi ya kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Dodoma leo Februari 27, 2024 kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Kuelekea Maadhimisho hayo, Mkoa kwa kushirikiana na Wizara husika umeandaa matukio mbalimbali kuanzia Machi Mosi, 2024 kuelekea siku ya kilele ambapo matukio hayo yatabeba dhima tofauti tofauti zinazolenga kumuinua na kumtangaza mwanamke.
Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Dodoma kitakachofanyika Machi 8, 2024 kwenye viwanja vya shule ya sekondari Chamwino, inatarajiwa kuhudhuriwa na Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB).
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.