MKOA wa Dodoma umefanya Mkutano wa wadau wa Elimu ikiwa ni kilele cha Juma hilo lililozinduliwa rasmi Machi 19. Mkutano huo umehudhuriwa na mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa TAG Mipango, Jijini Dodoma.
Lengo hasa la Mkutano huo ni kujadili namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu Mkoa wa Dodoma pamoja na kuweka mikakati ya kuinua Taaluma na ufaulu kimkoa pamoja na kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa Elimu Mkoa wa Dodoma.
Waziri Mkuu ameipongeza Dodoma kwa kuandaa Mkutano huo kwani unakwenda sambamba na Sera ya Elimu ya nchi.
"Kauli mbiu ya Mkutano huu inakwenda sambamba na Sera ya Elimu ya nchi inayosisitiza Uwajibikaji. Utoaji wa Elimu Bora ni vipaumbele vya nchi. Serikali yetu inaimarisha mazingira ya utoaji Elimu kwa kuboresha miundombinu na Elimu bila ada kwani mpaka Sasa shilingi Trilioni 1 zimetolewa kufanikisha hili.
"Niwasihi Maafisa Elimu Kata kufuatilia maendeleo ya shule zenu kila wakati kwa kuwatembelea walimu wenu na kusikiliza kero zao. Walimu nanyi hakikisheni munafanya tathmini ya uelewa wa wanafunzi kwa kuwapatia mazoezi mengi kadri inavyobidi. Fedha zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya Elimu, zitumike kwa ajili hiyo". Amesisitiza Majaliwa.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa DodomaRosemary Senyamule, amesema Serikali ya awamu ya Sita imefanya mambo mengi kwenye sekta ya Elimu.
"Tunamshukuru Rais kwa kuinua sekta ya Elimu Dodoma kwani tumeimarika sana miaka hii 3. Dodoma imepanda ufaulu wa darasa la 7 na kuingia kumi Bora kitaifa 2022 kwa ufaulu kupanda kutoka 83% (2022) hadi 87%(2023). Tumeanza kuweka mikakati ya Mkoa kuhakikisha kila mwaka ufaulu unapanda.
Pia ametaja mafanikio yaliyopatikana kipindi hiki kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya Elimu iliyogharimu shilingi Bilioni 92.4 , miradi ya BOOST shilingi Bilioni 10.6 iliyowezesha ujenzi wa Madarasa 196 na matundu ya vyoo 154. Fedha nyingine ni kutoka miradi ya SEQUIP, SWASH, TEA , EP4R na mingine mingi ambayo kwa pamoja imeboresha kiwango cha Elimu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.