• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Fidia uwanja Msalato, barabara za pete kuanza kulipwa

Imewekwa tarehe: May 10th, 2021

SERIKALI imesema kuwa itaanza zoezi la ulipaji fidia hivi karibuni kwa  wananchi wote waliochukuliwa maeneo yao ili kupisha miradi ya kimkakati ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato na barabara ya pete (mzunguko) ya jiji la Dodoma kwa njia nne (Km 112.3).

Aidha imeelezwa kuwa kiasi cha Shilingi Bilioni 12.7 imeshatolewa na kupelekwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa ajili ya fidia za mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma na kiasi cha shilingi Bilioni 14.5 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato. 

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Msalato na Matumbulu jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, amesema kuwa fidia hiyo italipwa kwa kuzingatia sheria na kusisitiza kuwa kila anayedai fidia hiyo atalipwa fedha yake yote.

“Leo nimekuja hapa kuwaeleza kuwa msiwe na wasiwasi juu ya fidia zenu, fedha zimepatikana na mtalipwa kwa mujibu wa sheria zote za nchi zilizopo, pia malalamiko yatasikilizwa kwa wale ambao hawataridhika”, amesema Waziri Chamuriho.

Dkt. Chamuriho amewaelezea wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuwa barabara hiyo itajengwa kwa sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza itahusisha Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (Km 52.3) na sehemu ya pili itaanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (Km 60) na tayari wakandarasi wa ujenzi wa sehemu hizo wameshapatikana.  

Amebainisha kuwa miradi hiyo ikikamilika itasaidia kuvutia fursa za uwekezaji  na hivyo kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa jiji la Dodoma na Taifa kwa ujumla.

Amewataka wananchi wa maeneo yanayopitiwa na miradi hiyo kutoa ushirikiano ili kurahisisha zoezi la ulipaji fidia kufanyika kama lilivyopangwa ili miradi hiyo ya kimkakati kuanza mapema na kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Selemani Kakoso, ameitaka Wizara kusimamia wakandarasi hao kikamilifu katika miradi hiyo na kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati kwa mujibu wa mikataba iliyowekwa.

Ametoa wito kwa wananchi wanaopitiwa na miradi hiyo kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa makandarasi na kuacha tabia ya kuhujumu miundombinu ili kupelekea miradi kukamilika kwa wakati.

Awali akitoa taarifa kwa Kamati, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, ameeleza kuwa mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko utahusisha pia ujenzi wa miradi mingine inayohusisha jamii moja kwa moja ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya vinne, visima vya maji vinne na magari matano ya kubebea wagonjwa.

Naye Mbunge wa Dodoma Mjini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, ameishukuru Serikali kwa kuamua kuanza utekelezaji wa miradi hiyo hivi karibuni kwani kukamilika kwa miradi hiyo kutapelekea kuchangamsha na kuleta maendeleo katika jiji la Dodoma.

Miradi ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko ya Dodoma (Km 112.3) kwa njia nne na Uwanja wa Ndege wa Msalato inafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa fedha za mkopo nafuu  kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


CHANZO:Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.