JUMLA ya wagonjwa 17500 wamepatiwa matibabu ya ugionjwa huo na Shirika linalotoa huduma za afya la CCBRT tangu shirika hilo lilipoanza kutoa huduma hizo mwaka 2003.
Meneja miradi wa Shirika la CCBRT,Yohana Kaswalala alisema hayo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambayo imefanyika kitaifa wilayani kasulu mkoani Kigoma na kusema kuwa jitahada zinapaswa kufanywa ili kukabiliana na tatizo hilo kwani bado ipo idadi kubwa ya waathirika hawajapata huduma.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa CCBRT,Brenda Msangi katika maadhimisho hayo Kaswalala alisema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kuna wanawake zaidi ya 500,000 kusini mwa Jangwa la Sahara wana matatizo ya Fistula kati yao 10,000 wakiwa nchini Tanzania.
Katika kukabiliana na hali hiyo alisema kuwa shirika hilo limeendelea kutoa matibabu bure na gharama za usafiri kutoka popote Tanzania kwenda katika hospitali yao jijini Dar es Salaam hivyo kutoa wito kwa wagonjwa wote kujitokeza kupata matibabu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Americares, Dk.Nguke Mwakatundu alisema kuwa changamoto ya Fistula nchini bado ni kubwa hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau hawana budi kufanya kazi kwa pamoja na kuongeza juhudi kukabiliana na tatizo hilo.
Dk.Mwakatundu alisema kuwa tangu mwaka 2011 shirika hilo lianzie kutoa huduma za afya limewezesha kupatiwa matibabu kwa wagonjwa 2000 katika hospitali ya Bugando na kubainisha kuwa kila mwaka wagonjwa 2500 wanatokea nchini na katibyaov wanaopata matibabu ni 1500 tu.
Mwakilishi huyo Mkazi wa Americares alisema kuwa ni lazima huduma za uzazi salama ziimatishwe sambamba na kusogezwa karibu kwa huduma za upasuaji kwa waathirika wa ugonjwa wa Fistula.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa afya, Ummy Mwalim alisema kuwa serikali imeazimia kutekeleza kwa vitendo mpango wa kuondoa tatizo la ugonjwa wa fistula kwa wanawake wakati wa kujifungua ifikapo mwaka 2030.
Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Tiba wizara ya afya, Profesa Pascal Rugajo alisema kuwa moja ya mipango mikakati katika kutekeleza hilo ni uwepo wa vituo vya kutoa huduma za uzazi salama na uzazi pingamizi ambavyo vimeonekana kuwa ndiyo chanzo cha matatizo ya Fistula.
Alisema kuwa hadi sasa huduma za uzazi salama zinatolewa kwenye vituo 503 nchini kwenye vituo vya afya na zahanati na kwamba serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutoa huduma kwa waathirika na kuongeza utoaji huduma ili ziweze kutolewa nchi nzjma kuwezesha kurudisha tabasamu kwa wanawake waliopatwa na tatizo hilo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.