• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Furahieni Makao makuu ya nchi yasiyo na kero ya Ardhi

Imewekwa tarehe: October 18th, 2023

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu yasiyokuwa na kero wala migogoro ya Ardhi.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi waliojitokeza kuhudumiwa na kutatuliwa kero zao katika Kliniki ya Ardhi iliyo katika siku yake ya tatu jijini Dodoma.

Senyamule alisema “niwahakikishie Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama mwenye upendo na mama anayewapenda watanzania, jambo hili halitaki na anatamani wananchi wa Dodoma wafurahie makao makuu ya Dodoma na watafurahia kama watapa haki zao. Ndiyo maana amekuwa akituagiza kutatua kero zao hasa za Ardhi katika Jiji la Dodoma. Kama mkoa baada ya kupokea maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wametuagiza kuhakikisha tunamaliza kero za Ardhi kwa wananchi wa Dodoma”.

Alisema kuwa mkoa umetengeneza mpango mkakati wa mwaka mmoja kuhakikisha kero za Dodoma zinaisha. “Kuanzia mwezi Julai hadi Desemba, 2023 kuna kero kubwa zinazogusa makundi makubwa tunaendelea kuzitatua. Kuanzia mwezi Januari hadi Juni, 2024 tunamalizia kero za mtu mmoja mmoja ambazo hazikukamilika kwa wakati. Nimpongeze Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mkurugenzi wa Jiji na Katibu Tawala Mkoa baada ya mkakati huu wameendelea kuunyumbulisha ili ukamilike vizuru wameongeza na ubunifu. Mfano kuanzisha hii Kliniki ya Ardhi ni moja ya mkakati wa kukamilisha kero kwa wakati” alisema Senyamule.

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kuzungumza na wananchi, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alisema kuwa timu ya wataalam imejipanga vizuri. “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tupo hapa tangu kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais, tusikae ofisini, tutoke kuwasikiliza wananchi na kero ya Ardhi kwenye jiji letu ni kubwa. Kutokana na ukubwa wake Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ulituongoza vizuri tukaandaa mkakati wa kushughulikia kero ya Ardhi. Mkakati mmoja wapo ni kuwa na kliniki za Ardhi, ambayo imeanzia hapa halmashauri na itakuwa ikihama kwenda maeneo ya kata kuwasilikiza wananchi” alisema Alhaj Shekimweri.

Katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alikabidhi Hati kwa wananchi 15 katika siku ya tatu ya utekelezaji wa Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.