Na. Asteria Frank, DODOMA
GARI la Darasa Tembezi kutoka Halmashauri ya Jiji Dodoma limetembelea Dodoma Media College kwa
lengo la kuelimisha kuhusu uandikishaji wa daftari la makazi kuelelea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Gari la darasa Tembezi limewapa wanafunzi wa chuo hicho elimu ya kujiandikisha kwenye daftari la
orodha ya makazi linaloanzaa 11-20 Oktoba,2024 na kuwataka washiriki katika uchaguzi wa serikali za
mitaa kwa maana ni haki yao na ni muhimu kuchaguwa viongozi wa mitaa wanayoishi
Mwenyekiti wa uelimishaji na uhamasishaji wa Darasa tembezi Shadia ……… aliwaelimisha wanafunzi
kuwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakao fanyika tarehe 27 Novemba, 2024 hivyo wanafunzi
wanatakiwa kujiandikisha kwenye daftari la makazi katika ofisi za Mitaa, Shule za Msingi na Sekondari,
zahanati na vituo vya afya, Maeneo ya wazi yenye mkusanyiko ya watu na majengo mengine ya Taasisi
za Umma yaliyopo katika Mitaa au Vitongoji ili aweze kushiriki kuchagua Mwenyeki pamoja na wajumbe
wa kamati ya utekelezaji.
Alisema kuwa kuna utofauti kati ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ambalo
lilikufanya upate kadi ya kupiga kura mwaka 2025 kwenye kuchagua Diwani, Mbunge na Raisi,
kujiandikisha kwenye daftari la makazi ni kwaajili ya kupata sifa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa na linabeba orodha ya wananchi wanaoishi katika eneo husika.
“Zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura haliusiani kabisa na uchaguzi wa
serikaliza mitaa kwahiyo ili kupata sifa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikari za Mitaa ni lazima ujiandikishe
kwenye daftari la mkazi katika mitaa tunayo toka” alisema ……...
Aliongeza kuwa kupata sifa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni lazima uwe Raia wa Tanzania,
uwe na umri wa miaka 18 na kuendelea , ni mkazi wa mtaa ambao uchaguzi unafanyika, uwe na akili
timamu na awe amejiandikisha kupigakura katika mitaa husika na zoezi la kujiandikisha ni la mda
mfupi.
Balozi wa Rushwa Noela …….. alisema kuwa ruswa ni kitendo cha kutoa au kupokea kitu chenye
thamani bila kufata taratibu au kwenda kinyume na sheria hivyo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa
na hata uchaguzi ujao mwakani vitendo vya ruswa vinachukua nafasi ikiwemo ruswa ya
ngono,manaweza kupewa hongo na vitu vingi sana.
“mimi kama balozi wa rushwa napenda kuwakataza msipokee wala msikubali kuchukuwa rushwa na
kama unaweza kukutana na tatizo kama hilo unawza kupiga 113 kwaajili ya kuripoti ukiwa na ushahidi
asanteni na ninawaomba msiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa” alisema Noel.
Mwanafuzi wa ngazi ya cheti wa Dodoma Media College Martin Tulo alisema kuwa uchaguzi wa serikali
za mitaa unatuhusu watu wote na watu tulikuwa na dhana ya kuwa wagombea wa uchaguzi ni ya watu
wenye umri mkubwa na wazee kumbe na sisi vijana tunapaswa kushiriki sio tu kupigakura hata
kugombea.
“kama vijana kuna faida nyingi zakushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa moja wapo ni kupata haki
yako ya msingi , kushiriki katika vikao vya maamuzi na pia kupata uzoefu wa uwongozi kwa wale
wanaotaka kuja kuwa wanasiasa hapo mbeleni” alisema Tulo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.