HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma imepata tuzo ya kutibu wagonjwa wa mifupa waliovunjika kwa kutumia vyuma va kisasa (SIGN NAIL) kwa mwaka 2021.
Tuzo hiyo imetolewa na Mtandao wa watengeneza vyuma vya kutibia mifupa ya nchini Marekani.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ilikuwa ya kwanza Duniani kwenye program hiyo iliyoanza mwaka 1999 na sasa kuna zaidi ya Hospitali 300 duniani zinazotibu kwa SIGN nail (SURGICAL IMPLANT GENERATION NETWORK).
Hospitali hiyo ya Rufaa ilianza kutumia vyuma hivi mwaka 2016 na mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 3,000 wamefaidika na huduma hii tokea hospitali ianze kutumia vyuma tiba hivyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.