WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia hakuna wagonjwa wapya wa Marburg walioripotiwa licha ya kupokea tetesi sehemu mbalimbali mkoani hapa.
Hayo ameyasema alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ambapo ameambatana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani Dkt. Zabron Yoti na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNICEF Bi. Shalini Bahuguna
"Tangu kuanza kwa ugonjwa huu hadi leo tumeendelea kuwa na jumla ya wagonjwa walewale Nane waliothibitika ambapo Watano kati yao walifariki na Watatu wanaendelea na matibabu katika vituo vya kutolea huduma vilivyoainishwa.”" amesema Waziri Ummy
Aidha, waziri Ummy amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Wadau mbalimbali inaendelea kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu kwa kutekeleza mikakati mbalimbali.
"Miongoni mwa hatua ni kuwaweka sehemu maalumu watu wote waliohudumia wagonjwa ambao ni wanafamilia waliouguza wagonjwa na watumishi wa Afya kwa siku 21 ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu kama watabainika na maambukizi." amesema Waziri Ummy
Katika kuendelea kudhibiti ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeongeza wataalam Sita wa afya ikiwemo daktari bingwa bobezi wa magonjwa ya Figo, daktari bingwa wa magonjwa ya ndani na wauguzi waliopata mafunzo maalumu kutoka maeneo mengine ili kusaidiana na wataalamu wa afya Mkoani Kagera.
Pia, Waziri ummy amewatoa hofu wananchi kuwa waendelee na shughuri zao na amewakumbusha juu ya kuendelea kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kupeana nafasi na kuacha kugusana.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.