• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Kilele Mbio za Mwenge wa Uhuru Lindi, Serikali inamuenzi Mwl. Nyerere - JPM

Imewekwa tarehe: October 14th, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU) kufanya uchunguzi kwa miradi 107 yenye thamani ya shilingi Bilioni 90.28 iliyobainika wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu (2019) kuwa na dosari mbalimbali zikiwemo kutekelezwa chini ya ubora, kutokamilika, matumizi mabaya ya fedha za umma na udanganyifu.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 14 Oktoba, 2019 katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika Kitaifa katika uwanja wa Ilulu Mjini Lindi.

Mhe. Rais Magufuli amekabidhi kitabu cha taarifa ya miradi hiyo kilichowasilishwa kwake na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu Bw. Mzee Mkongea Ali kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brid. Jen. John Mbungo na kumuagiza wote watakaobainika kuhusika katika dosari za miradi hiyo kufikishwa Mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake.

Katika taarifa hiyo Bw. Mzee Mkongea Ali amesema udanganyifu mkubwa umebainika katika miradi ya maji na amesisitiza endapo fedha vyingi zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kutatua tatizo la maji zitasimamiwa vizuri, tatizo hilo litapata ufumbuzi.

Amebainisha kuwa yeye na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wenzake wamebaini kazi kubwa inayofanywa na Serikali ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, kuongezeka kwa nidhamu katika utumishi wa umma na kujengwa kwa miundombinu muhimu ya kuvutia uwekezaji.

Kabla ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa hajasoma risala ya wananchi wa Tanzania, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenister Mhagama amesema mwaka huu Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa miezi 7 katika jumla ya kilometa 26,274 ambapo umeweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi ya maendeleo 1,390 yenye thamani ya shilingi Trilioni 4 na Bilioni 750 iliyopo katika Mikoa 31 na Halmashauri 195.

Kuhusu kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mw. Julius Kambarage Nyerere, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kumuenzi kwa kutekeleza kwa vitendo misingi ya Uhuru na Azimia la Arusha ambalo linahimiza watu kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, elimu kwa wote hasa elimu ya ufundi, kupiga vita umasikini na ukosefu wa ajira, kujenga miundombinu, uzalendo na nidhamu kwa watumishi wa umma.  

Ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itajitahidi kwa kadri iwezavyo kumuenzi Baba wa Taifa na ametaja baadhi ya juhudi zilizofanywa kwa vitendo kuwa ni kupambana na rushwa ambapo Mahakama ya kushughulikia Ufisad imeanzishwa, watumishi hewa takribani 20,000 na wafanyakazi wenye vyeti feki 14,000 wameondolewa katika utumishi wa umma, kutoa shilingi Bilioni 470 kwa mwaka kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu, kuboresha huduma za afya ambapo hospitali mpya 69 na vituo vya afya 352 vinajengwa na kuongeza bajeti ya dawa kutoka shilingi Bilioni 31 hadi kufikia Bilioni 270.

Maeneo mengine ni kuboresha upatikanaji wa huduma za maji Mijini na Vijijini ambapo takribani shilingi Trilioni 2 zinatumika, kuhimiza ujenzi wa viwanda ambapo viwanda takribani 4,000 vimejengwa, kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa ujenzi wa Bwawa la Mwl. Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 za umeme ambapo shilingi Trilioni 6.5 zinatumika, kujenga reli ya kisasa (standard gauge railway - SGR) ambapo shilingi Trilioni 7.3 zinatumika, kujenga viwanja vya ndege 11, kununua ndege 11, kupanua bandari ambapo takribani shilingi Trilioni 1 zinatumika, kununua meli mpya na kukarabati za zamani.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali za Awamu ya Tano inamuenzi Baba wa Taifa kwa kuhakikisha inasimamia vizuri rasilimali na maliasili zikiwemo misitu, wanyamapori na madini kupitia sheria mpya ya mwaka 2017 ambayo imewezesha kuongezeka kwa mapato ya madini kutoka shilingi Bilioni 191 mwaka 2016/17 hadi kufikia shilingi Bilioni 335 mwaka 2018/19, kuanzisha Hifadhi za Taifa 4 ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Nyerere baada ya kumega Pori la Akiba la Selous na kuimarisha sekta ya Kilimo.

Kuhusu vijana, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Serikali ya Awamu ya Nne iliyoongozwa na Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa na ameahidi kuwa Serikali ya Awau ya Tano itaendeleza mafunzo hayo.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziba Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri wa Tanzania Bara na Zanzibar, Mabalozi, Wakuu wa Mikoa na viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Kesho tarehe 15 Oktoba, 2019 Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Lindi ambapo atazindua barabara za Mji wa Rungwa, ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa ghala za mazao la Kijiji cha Lipande Wilayani Ruangwa na atahutubia mkutano wa hadhara Mjini Ruangwa.

Chanzo: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.