Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepokea zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya elimu ya msingi kutoka kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi wa Mikutano ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waandishi wa Habari katika kampeni ya Tumekusikia Tumekufikia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Kayombo alisema “kwa upande wa elimu ya msingi, tumepokea zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya elimu ya msingi. Tumepokea shilingi bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya tatu ambazo ujenzi unaendelea”.
Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa program hiyo ni muhimu kuzungumzia maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini. “Serikali ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imekusikia imekufikia, wale wafanyakazi waliokaa miaka kadhaa mshahara haujapanda tumekusikia tumekufikia, wale waliokuwa wanateseka na maji safi na salama hayapo, tumekusikia tumekufikia, wale ambao ilikuwa ni lazima kumsafirisha mgonjwa wake kumpeleka Dar es Salaam kwenda kutibiwa tumekusikia tumekufikia, ni kampeni rahisi na inaeleka” alisema Waziri Nnauye.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.