Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia kitengo cha Ustawi wa Jamii wametoa vitu mbali mbali kwa ajili ya Watoto yatima wa Kituo cha Hope of Charity kilichopo kata ya Hombolo Bwawani.
Mratibu wa zoezi hilo Rebeka Ndaki ambaye ndiye mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii amesema vitu vilivyotolewa ni pamoja na nguo, viatu, sabuni, na mahitaji mengine mbalimbali ambapo watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma walivitoa kwa hiari yao kwa ajili ya zawadi ya sikukuu Noel na mwaka mpya.
Kitengo cha Ustawi wa Jamii kimekuwa na utaratibu wa kuwatembelea watu mbalimbali wenye mahitaji kwa nyakati tofauti kama namna mojawapo ya kutekeleza majukumu yake kwa jamii.
Nao watoto waliopatiwa msaada huo katika kituo cha Hope of Charity wameishukuru menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na watumishi wake kwa kuwakumbuka na kushiriki pamoja nao katika kusherehekea sikukuu ya Krismas na pia kuwawezesha kupata mahitaji hayo ya kijamii.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.