• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Halmashauri zaagizwa kuweka mikakati kupandisha ufaulu

Imewekwa tarehe: March 15th, 2021

KATIKA kuhakikisha kiwango cha ufaulu kwa shule za Msingi na Sekondari kinapanda kwa Mkoa wa Dodoma kila halmashauri imetakiwa kuweka mikakati mizito na kuifuatilia kwa kina ikiwamo kuwashirikisha wazazi na wadau wa elimu katika kufikia malengo ya kupandisha ufaulu kwa mkoa huo.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma wakati akiwasilisha tamko la Mkoa katika kikao cha wadau wa elimu katika Mkoa huo waliokutana kwa lengo la kushirikishana mbinu katika kuboresha elimu ya Mkoa ili kupandisha kiwango cha ufaulu.

Amesema ni lazima kila Halmashauri kuhakikisha inakuwa na mkakati sambamba na kuupangia bajeti ili kuweza kupunguza kiwango kufeli kwa wanafunzi na kushughulikia vikwazo vyote vinavyopelekea Watoto kushindwa kuzingatia masomo na kushindwa kufaulu.

“Kila halmashauri kuwe na ufuatiliaji wa kina wa ufundishaji wa kila shule na kila mwalimu, Mkuu wa Wilaya asimamie Wakurugenzi wake na Mkurugenzi asimamie wakuu wa idara hadi ngazi za chini tunataka ufaulu upande hapa tulipo ni aibu tupu” amesema Maduka.

Amesema Dodoma ya sasa si Dodoma ya miaka mitano ya nyuma kwa sasa Dodoma ni Mkoa wa kisera na utawala hivyo ni aibu kuona Mkoa ukishika nafasi za chini katika kiwango cha ufaulu amebainisha kuwa wameweka mikakati mbalimbali baada ya miaka mitatu wawe nafasi ya 15 na 2025 kuwa namba chini ya 10 kitaifa.

Ameongeza “Katika halmashauri zetu tunataka ziondoke huko kwa sasa na kila Halmashauri lazima iwe chini ya 100 kitaifa ili kiwango cha kimkoa kipande yote haya yatafanikiwa ufuatiliaji wa kina kila ngazi ukifanyika” amesema.

Amesema kila Halmashauri ziweke utaratibu wa kuweka mikutano na wazazi ili kuwashirikisha katika mambo mbalimbali na siku hiyo itumike kusoma matokeo ya wanafunzi ili mzazi wake ajue nafasi yam toto wake hiyo itaweza kusaidia kuongeza hamasa kwa wazazi kuwasimamia Watoto na Watoto kuongeza kujituma katika masomo.

Katika tamko hilo limetaka Halmashauri zenye shule na wanafunzi wake wanazidi wanafunzi 800 kwa shule ya Msingi na wanafunzi 500 kwa shule za Sekondari kuanza kujiandaa kujenga shule nyingine au kujenga shule shikizi na katika chumba kimoja cha darasa kwa shule za msingi wasizidi wanafunzi 50 na kwa Sekondari wasizidi 40.

Amesema ili kufikia malengo ni lazima kila robo ya mwaka kufanyika kwa tathmini ya maendeleo kwa kila Halmashauri ili kushirikiana katika changamoto zilizopo katika kutekeleza hayo kufikia malengo yaliyowekwa ya kuongeza ufaulu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge wakati akifungua kikao hicho amewataka wakuu wa Wilaya na wakurugenzi kwenda kusimamia hayo sambamba na kuwasimamia waratibu wa shule na kuwa wabunifu katika kutekeleza tamko hilo.

Ameongeza kuwa “ tutakuwa tukikutana na kamati kutathmini nini kimefanyika Chemba na nini kimefanyika Kondoa lengo letu ni kuhakikisha haya tunayokubaliana yanatekelezeka na mnapokutana na ugumu wowote tushirikishane lengo tufike tulipopataka” amesema Dkt Mahenge.

Katika kikao hicho Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema kuna haja ya kufanyika tathmini kwani viongozi wengi ngazi ya kata hawatekelezi majukumu yao hivyo wafuatiliwe ili watekeleze majukumu yao kikamilifu.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.