Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapongeza na kuwatakia heri Watanzania wote kwa sikukuu ya Krismas na amewataka kuendelea kumshukuru Mungu kwa miujiza na upendo mkubwa anaolitendea Taifa la Tanzania.
Mhe. Rais Magufuli amesema upendo na miujiza ya Mungu kwa Tanzania inajidhihirisha katika kipindi hiki ambapo dunia inapita katika wakati mgumu wa janga la ugonjwa wa Korona (Covid-19) ambapo maelfu ya watu wanaendelea kupoteza maisha kila siku duniani, lakini Tanzania imeepushwa na janga hilo na maisha ya Watanzania yanaendelea kama kawaida.
Amewaomba Watanzania wote waendelee kumshukuru Mungu na kumuomba aendelee kulilinda Taifa lao dhidi ya ugonjwa huo, na kuwaombea wananchi wa Mataifa mengine waepushwe na Korona.
Mhe. Rais ametoa wito kwa viongozi wa Mataifa mbalimbali duniani kukubali kumweka Mungu mbele katika mapambano dhidi ya Korona badala ya kuendelea kutegemea nguvu za binadamu pekee.
Pamoja na kuwatakia heri ya Krismas, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi za uzalishaji mali ili kuendelea kujenga Taifa lao pamoja na kuhakikisha wanamtanguliza Mungu kwa kila jambo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.