• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Hongera Jiji la Dodoma kwa kununua mitambo ya kufungua barabara - DC Shekimweri

Imewekwa tarehe: September 18th, 2022

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa kusimamia maazimio ya vikao yanayolenga kutatua changamoto zinazoigusa jamii kwa kununua mitambo miwili ya kufungua barabara katika maeneo yaliyopimwa viwanja ili kuwarahisishia wananchi shughuli za ujenzi.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri kabla ya uzinduzi wa awali wa mitambo miwili kwa ajili ya ufunguzi wa barabara katika maeneo mbalimbali yaliyopimwa viwanja tukio lilifanyika katika kiwanda cha kuzalisha tofali za gharama nafuu Kata ya Kizota jijini Dodoma.

Shekimweri aliipongeza Halmashauri ya Jiji kwa kutekeleza maazimio ya vikao vya kisheria vinavyolenga kutatua changamoto zilizopo katika jamii. “Nawapongeza kwa uthubutu na kusimamia maazimio yenu ya vikao vya kisheria, Kamati ya Fedha na Utawala na Baraza la Madiwani ambao waliainisha umuhimu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa na mitambo yake yenyewe kwa ajili ya kutekeleza miradi yake kwa gharama nafuu.

Naona mnaendeleza alama ambayo Jiji la Dodoma limejiwekea katika matumizi ya fedha za mapato ya ndani. Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni miongoni mwa halmashauri chache nchini ambazo mapato yake ya ndani yanaacha alama. Tunafahamu mnafanya hayo kwa kuzingatia miongozo ya kibajeti, lakini sisi Jiji la Dodoma huu ni utashi wetu wa kujihoji na kuacha alama kubwa kwa bajeti tunayoacha katika mwaka wa fedha husika” alisema Shekimweri kwa kujiamini.

Akiongelea umuhimu wa mitambo hiyo kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na wananchi kwa ujumla, alisema kuwa mitambo hiyo itasaidia kufungua barabara katika maeneo yaliyopimwa viwanja. “Mitambo hii pamoja na kufungua barabara pia itasaidia kuweka mandhari ya jiji vizuri na kuongeza thamani ya maeneo husika. Barabara zikifunguliwa zitasaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwa sababu wananchi wanashindwa kuendeleza viwanja vyao kutokana na viwanja hivyo kutofikika kirahisi. Hivyo, mitambo hii ni suluhisho kwa wananchi.” alisema Shekimweri.

Akiwasilisha taarifa ya ununuzi wa mitambo miwili kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema kuwa mitambo hiyo inaenda kutatua migogoro inayoendelea katika jiji hilo ya wananchi kujenga maeneo ya barabara kutokana na kutokuwa na barabara zilizofunguliwa. Alisema kuwa halmashauri imepima zaidi ya viwanja 700,000 kwa upimaji shirikishi, utwaaji na urasimishaji. “Kilio cha wananchi kimekuwa ni baada ya kupima viwanja lini barabara zitafunguliwa na kuchongwa. Halmashauri ina barabara zenye urefu wa kilometa 1,768 zinazotakiwa kufunguliwa” alisema Mkurugenzi Mafuru.

Akiongelea gharama za ununuzi wa mitambo hiyo, Mkurugenzi Mafuru alisema kuwa mitambo hiyo imegharimu shilingi 1,818,716,300. Aliitaja mitambo hiyo kuwa ni Greda (140K) limegharimu shilingi milioni 943.5 na Buldoza (D6) limegharimu shilingi milioni 863.33 na usafiri kutoka Dar es salaam hadi Dodoma uligharimu shilingi 11,800,000.

Mkurugenzi huyo aliyataja maeneo ambayo yanauhitaji mkubwa wa kufungua Barabara kuwa ni Ndachi Mnadani, Michese, Nala Lugala, Zuzu, Iyumbu, Ngh’ong’ona, Mkonze, Makutopora, Ntyuka, Nala Chihoni, Mbwanga, Veyula, Msalato, Hombolo na Miyuji.

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde alilishukuru Baraza la Madiwani na Menejimenti ya jiji kwa kuona umuhimu wa kuwa na mitambo hiyo. “Nachukua nafasi hii kupongeza hatua hii kubwa iliyofikiwa. Naamini wananchi wanakwenda kutatuliwa migogoro yao na maeneo yaliyokuwa hayafikiki, sasa yanakwenda kufikika” alisema Mavunde.

Akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Jamal Ngalya alimhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kuwa usimamizi mzuri wa Baraza la Madiwani na Menejimenti kwa mitambo hiyo. “Mheshimiwa mkuu wa wilaya mitambo hii tutaisimamia vizuri na kuratibu matumizi yake. Lakini Mhehsimiwa mkuu wa wilaya tunakupongeza na wewe kwa usimamizi wako madhubuti” alisema Ngalya.

Mmoja ya mitambo iliyonunuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukifanyiwa majaribio.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.