• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Imarisheni ulinzi wa vifaa vipya vya TEHAMA mashuleni – Waziri Mchengerwa

Imewekwa tarehe: February 7th, 2024

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na kufikisha kwenye vituo teule vifaa vya TEHAMA vilivyogawiwa kwa vituo zaidi ya 800 kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST).

Mchengerwa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa vituo vya walimu na Shule za awali na Msingi uliofanyika Jijini Dodoma.

"Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri imarisheni ulinzi na usalama katika shule zitakazopokea vifaa vya TEHAMA na ndani ya siku tatu vifaa hivi viwe vimekabidhiwa kwa mikoa husika.

Amewataka kuhakikisha shule zinazopelekewa vifaa zisibadilishwe labda kwa kibali maalumu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amewataka watendaji hao kusimamia matumizi ya vifaa hivyo ili kuleta mapinduzi makubwa katika eneo la ujifunzaji na ufundishaji na kwamba yeye mwenyewe atapita kukagua utekelezaji wake lakini pia matarajio ya Serikali ni kuongeza vifaa zaidi ili shule zote ziweze kufikiwa.

Mchengerwa amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za dhati katika kuboresha sekta ya elimu nchini

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Franklin Rwezamula ameipongeza Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kununua vifaa vya TEHAMA kupitia Mradi wa Kukuza Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) kwa lengo la kuimarisha vituo vya walimu (TRC) na shule zilizoteuliwa kama sehemu muhimu ya kutolea Mafunzo endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) na kuwezesha zoezi la Ufundishaji na Ujifunzaji kwa wanafunzi ambao watatumia vituo hivyo zaidi ya 800

Aidha, amesema Wizara ya elimu itaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 ambayo sasa ipo katika utekelezaji wake kwenye mitaala iliyoboreshwa hapa nchini.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.